Mkutano kati ya Ujerumani na Urusi | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.07.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano kati ya Ujerumani na Urusi

Rais wa Urusi, Dmitr Medvedev amekutana na Kansela Angela Merkel mjini Hannover Ujerumani kwa kikao cha pande mbili cha siku mbili

default

Rais wa Urusi Dmitr Medvedev na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel

Rais wa Urisi Dmitr Medvedev amewasili nchini Ujerumani hapo jana kwa mazungumzo na Kansela Angela Merkel.

Deutsch-russische Regierungskonsultationen: Merkel und Medwedew

Ni mkutano unaofanyika kila mwaka kati ya nchi hizo mbili

Viongozi hao wanakutana katika mji uliopo kaskazini, Hanover, kwa kikao cha pande mbili cha siku mbili. Ni mkutano wa 13 wa kila mwaka wa viongozi wa kisiasa na kibiashara kutoka nchi hizo mbili.

Huenda uhusiano unaokuwa wa kibiashara kati ya Ujerumani na Urusi ndio ukatawala kikao hicho. Ujerumani ni mshirika wa kipekee wa muhimu kibiashara kwa Urusi ,na Urusi ni muuzaji mkubwa wa nje wa nishati kwa Ujerumani.

Mwandishi:Maryam Abdalla/afp, dapd

Mhariri:Kitojo Sekione

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com