Mkurugenzi IMF achunguzwa | Habari za Ulimwengu | DW | 19.10.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mkurugenzi IMF achunguzwa

Washington:

Shirika la fedha la kimataifa IMF limeanza uchunguzi dhidi ya Mkurugenzi wake mkuu Dominique Strass-Kahn kwa matumizi mabaya ya madaraka. Uchunguzi huo unatokana na madai ya uhusiano aliokua nao Bw Strauss-Kahn mwanzoni mwa mwaka huu na hawara yake ambaye sasa si mfanyakazi tena wa Shirika hilo. Kwa mujibu wa ripoti ya Jarida la Wall Street hawara huyo alikua afisa wa ngazi ya juu katika idara ya Afrika ya Shirika hilo. Bw Strauss-Kahn waziri wa zamani wa fedha wa Ufaransa amesema katika taarifa yake kwamba anashirikiana na walioajiriwa na Shirika hilo la fedha kuchunguza madai hayo. Uchunguzi huo unafanyika mwaka mmoja baada ya Rais wa zamani wa Beni ya dunia Paul Wolfowitz kulazimika kujiuzulu kuhusiana na kisa cha kuamuru kupandishwa cheo na malipo ya juu ya mshahara kwa hawara , aliyekua akifanya kazi

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com