1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa kutoshambuliana kati ya waasi wa LRA na majeshi ya serikali ya Uganda unamalizika Ijumaa Febuari 29

Kalyango Siraj28 Februari 2008

Je! Mkataba huo utarefushwa tena?

https://p.dw.com/p/DFUj
Joseph Kony ,kiongozi wa kundi la waasi wa Lord Resistance Army-LRA.Mkataba wa kutoshambuliana kati ya wapiganaji wake na wanajeshi ya serikali wa UPDF unamalizika Ijumaa 29Picha: AP Photo

Mkataba wa mda wa kutoshambuliana kati ya majeshi ya serikali ya Uganda na waasi wa Lord Resistance Army-LRA unamalizika kesho Ijumaa Febuari 29.Mda huo unakaribia wakati kukiwa na matumaini ya pande mbili husika katika mgogoro wa miaka mingi huenda kufikia muafaka.Hata hivyo baado kuna tatizo la waranta wa kukamatwa kwa viogogo wa chama cha LRA.

Makubaliano ya kusitisha hujuma kati ya majeshi ya serikali Uganda dhidi ya waasi wa LRA wakiongozwa na Joseph Kony yamerefushwa mara kadhaa.

Makubaliano ambayo yanamalizika hapo kesho yalirefushwa januari 30 mwaka huu-baada ya kurefushwa mara kadhaa na serikali ya Uganda ambayo imepigana vita dhidi ya kundi hilo kwa kipindi cha miaka 22.

makubalianoa hayo yalitiliwa saini mara ya kwanza Agosti mwaka wa 2006.

Kwa ujumla mapatano ya kutoshambuliana yamekuwa yanaheshimiwa kwa njia moja na waasi hao wa LRA ambao wameendesha vita vya chini kwa chini kwa miongo miwili na kulaumiwa kwa vifo vya raia wa Uganda mamia kwa maelf.

Kundi hilo licha ya kuwa limekuwa likiheshimu mapatanao hayo lakini linasema kuwa halitasaini mkataba wa amani ikiwa mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ya mjini The hague Uholanzi, haitafutilia mbali waranta wa kukamatwa kwa vigogo wa kundi hilo.

Wajumbe wa kundi hilo katika mazungumzo ya kuleta amani yanayoendelea mjini juba kusini mwa Sudan waliitaka serikali ya Uganda kuiondoa kesi yao ilioko mbele ya mahakama ya kimataifa kwa viongozi wa kundi hilo ili amani kuweza kupatikana.

Wajumbe wa waasi na wa upande wa serikali walitia sahihi makubaliano kadhaa wiki iliopita-hatua ilioleta matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa amani na hivyo kumaliza mgogoro ambao umechukua mda mrefu.Umekuwa ukiendelea kwa mda wa miaka 22.

Kiongozi wa ujumbe wa LRA kwenye mazungumzo-David Nyekorach Matsanga aliliambia shirika la habari la Reuters mjini juba kuwa upande wao hautaendelea na kutia saini mkataba wa amani hadi pale serikali ya Uganda itakapoomba Umoja wa Mataifa kufuta waranta wa kukamatwa kwa makamanda wajuu wa kundi hilo.

Kundi hilo linalaumiwa kwa kuwauwa raia wasio na silaha,kuwakata viungo wananchi,kuwachukua mateka watoto na baadae kuwatumia wasichana aidha kama wachumba ama kama wapiganaji ,wengine kama watumwa.

Lakini msemaji wa ujumbe wa serikali katika mazungumzo hayo-Chris Magezi,yeye alipinga madai ya wajumbe wa LRA akisema kuwa hilo haliwezekani ikiwa kiongozi wa LRA hayuko mikononi mwao.

Mapema wiki hii serikali ya Uganda ilisema inataka mkataba wa amani utiwe saini tarehe 6 mwezi wa machi.

Wao waasi wanasema hawana haja ya kuharakisha,kwani wanahitaji mda zaidi kuwasiliana na kiongozi wao Joseph Kony ambae kwa sasa yuko katika maeneo ya mpaka wa Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Wakati waasi wakitaka mda zaidi kwa ushauriano-haijulikani ikiwa mda zaidi wa kutoshambulina utasogezwa mbele na serikali.Serikali imekuwa ikiililaumu kundi hilo kwa kuvunja vipengelee vya makubaliano hayo kama vile vigoo wa chama hicho kutokusanyika katika maeneo ya Ri Kwangba katika mpaka wa Sudan na Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Na badala yake wao wako katika mbuga ya wanyama ya Garamba ndani mwa Kongo.

Hata hivyo hatua ya mwisho inatarajiwa kutoka kwa serikali ya Uganda.