1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nachfolgeabkommen

Sekione Kitojo4 Desemba 2009

Leo Jumamosi tarehe 5.12 mkataba wa kupunguza silaha baina ya Marekani na Urusi ujulikanao kama START unamalizika muda wake.

https://p.dw.com/p/KqXP
Rais wa Marekani Barack Obama akizungumza mjini Florida nchini Marekani.Picha: picture-alliance/ dpa

Leo Jumamosi tarehe 5.12 mkataba wa kupunguza silaha baina ya Marekani na Urusi unaojulikana kama START unamalizika muda wake. Mkataba ambao hapo Julai 1991 marais wa zamani George Bush wa Marekani na Mikhail Gorbatschow wa Urusi walitia saini zao. Baada ya kuidhinishwa na baraza la Seneti la Marekani na bunge la Urusi Duma mkataba huo ulianza kazi rasmi tarehe 5 Desemba 1994. Mazungumzo bado yanaendelea mjini Geneva kati ya Marekani na Urusi kuhusu mkataba mpya.

Katika mkataba wa START Marekani na Urusi zimechukua jukumu la kupunguza hazina ya silaha zao za kinuklia , ambazo zimekuwa tangu kuanza kwa vita baridi mwanzoni mwa miaka ya 50 zikitumika kutishiana. Idadi ya makombora, yanayoweza kurushwa kutoka ardhini , makombora ya masafa marefu kuanzia zaidi ya kilometa 5,500, nyambizi pamoja na ndege za kivita zinazo beba mabomu zitapunguzwa kwa kiasi cha 1,600 kila kundi.

Idadi ya silaha zenye kubeba vichwa cha kinuklia zinapaswa kwa wastani kufikia kiasi cha 6,000 tu. Nchi zote mbili katika muda wa miaka 15 iliyopita zimeweza kupunguza silaha zao za kinuklia kwa kiasi cha jumla ya silaha 2,200.

Tangu mwezi Mei mwaka huu Marekani na Urusi zinajadiliana mjini Geneva kuhusiana na mkataba utakaochukua nafasi ya mkataba unaomalizika wa START, ili kuweza kupunguza zaidi silaha hizo za kinuklia.Mwanzoni mwa mazungumzo hayo ya kupatikana mkataba mpya rais wa Marekani Barack Obama alitoa hotuba mjini Prag, ambapo kama rais wa kwanza wa Marekani tangu mwanzo wa mashindano ya kinuklia na shambulio la bomu la kinuklia lililofanywa na majeshi ya Marekani katika miji ya Horoshima na Nagasaki mwaka 1945 ameanzisha harakati duniani za kuleta amani kwa kutaka dunia iachane na silaha za kinuklia.

Nasema wazi na kuamini kuwa Marekani ina nia ya kutaka kuwa na dunia yenye amani na usalama bila ya silaha za kinuklia.

Kama hatua sahihi kuelekea katika njia ya kuweza kutimiza msimamo huu rais wa Marekani alianzisha mazungumzo ya kupatikana mkataba utakaochukua nafasi ya makataba wa START. Mwezi Julai mwaka huu rais Obama pamoja na mwenzake rais Dmitri Medvedev wa Urusi walikubaliana malengo ya mkutano wa Geneva kwa kila upande.

Mkataba mpya unataka kuweka kiwango cha juu cha makombora ya kinuklia kuwa 1,675 na vifaa vya kurushia makombora kufikia 1,000.

Ikiwa mambo yote yatakwenda sawa , ikulu ya Marekani inataka sherehe za utiaji zifanyike katika mji mkuu wa Iceland, Reykjavik, mahali mbapo mwaka 1986 marais Mikhail Gorbatchov na Ronald Regan walikaribia kupata maafikiano ya mwanzo ya kupunguza silaha hizi za atomic.

Marekani kutokana na kumalizika kwa mkataba huu wa START inapaswa kufunga kituo chake cha uchunguzi kilichoko kilometa 600 mashariki ya mji wa Moscow, ambapo kutokea hapo wachunguzi wa kimarekani walikuwa wakiangalia utengenezaji wa kombora la kisasa la Urusi la Topol-M pamoja na silaha nyingine.

Kwamba hatua muhimu ya kwanza kuelekea katika dunia bila ya kuwa na silaha za kinuklia ni suala gumu, na inawezekana kushindwa, Obama tayari amelizungumzia katika hotuba yake mjini Prag April mwaka huu.

Sio kwamba mie ni mjinga. Lengo hili halitafikiwa haraka, huenda sio katika wakati wa uhai wangu. Linahitaji uvumilivu na hali ya kuendelea.

Na kwamba Urusi imekwisha ondoa kituo chake cha uchunguzi nchini Marekani muda mrefu uliopita, haitakubali katika mkataba huu mpya kuwekewa tena kituo cha uchunguzi ili kuidhibiti.

Mwandishi : Zumach, Andreas / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Abdul-Rahman