1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkanganyiko wa Rasimu ya Katiba Tanzania

Mohammed Khelef11 Oktoba 2014

Wakati Bunge Maalum la Katiba likimaliza vikao vyake na kukabidhi kile kinachoitwa "Rasimu ya Katiba Inayopendekezwa", maswali yanayozuka ni pamoja na hatima ya Tanzania ndani ya rasimu hiyo tata.

https://p.dw.com/p/1DTYr
Baadhi ya wananchi wa Tanzania wakihudhuria moja ya mikutano ya kampeni za uungaji mkono Rasimu ya Pili iliyotolewa na Tume ya Warioba.
Baadhi ya wananchi wa Tanzania wakihudhuria moja ya mikutano ya kampeni za uungaji mkono Rasimu ya Pili iliyotolewa na Tume ya Warioba.Picha: DW/M.Khelef

Rasimu ya Katiba Iliyopendekezwa na Mustkabali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio mada ya mazungumzo Mbele ya Meza ya Duara ya Idhaa ya Kiswahili ya DW Bonn. Kuijadili mada hiyo ni Salmin Awadh (mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi na aliyekuwa Mbunge wa Bunge Maalum kutoka Zanzibar), Ally Saleh na Humphrey Polepole (waliokuwa mjumbe wa Tume ya Warioba) na Gwappo Mwakatobe, mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Tanzania. Muongozaji ni Mohammed Khelef na swali kuu ni: Je, Tanzania inaelekea wapi baada ya Rasimu Iliyopendekezwa?

Kusikiliza mjadala wote, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Mohammed Khelef
Mhariri: Caro Robi