1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Mjumbe wa UM kwa Kongo atahadharisha kutanuka kwa mzozo

10 Julai 2024

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Bintou Keita amesema kuna "kitisho cha dhahiri" cha kusambaa kwa mzozo unaendelea mashariki mwa nchi kati ya jeshi la taifa na waasi wa M23.

https://p.dw.com/p/4i6Ug
DR Kongo | Umoja wa Mataifa | Bintou Keita.
Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Bintou Keita.Picha: Bianca Otero/ZUMA Wire/IMAGO

Katika ripoti yake aliyoiwasilisha mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Bibi Keita ametahadharisha juu ya kutanuka kwa maeneo yanayoshikiliwa na waasi wa M23 kwenye mkoa Ituri kama moja ya sababu za kutia hofu. 

"Kusogea kwa uwanja wa mapambano na uwepo wa silaha nzito za kivita katika maeneo yanayozunguka kambi za wasio na makaazi vinauweka rehani usalama wa watu waliokimbia mapigano na wakaazi wa maeneo hayo" Alisema Keita.

Vile vile ripoti yake imeitaja Rwanda kuwa imeongeza uungaji wake mkono kwa waasi wa M23.

Soma pia:UN: Vikosi vya Rwanda vyasaidiana na M23 kupigana Kongo

Hivi karibuni ripoti ya jopo la wataalamu wa Umoja wa Mataifa ilisema zaidi ya wanajeshi 4,000 wa Rwanda wako ndani ya mipaka ya Kongo na wamekuwa wakihusika kupanga mashambulizi.