1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mji wa Pyeongchang kuwa mwenyeji wa michezo ya Olympics 2018

Halima Nyanza(ZPR)7 Julai 2011

Wakorea kusini usiku wa kuamkia leo wamesherehekea kwa kurusha fataki angani, baada ya nchi hiyo kutangazwa rasmi kuwa mwenyeji wa michezo ya Olympic ya majira ya baridi mwaka 2018.

https://p.dw.com/p/11qdn
Mkuu wa kamati ya Kimataifa ya Olympic Jacques Rogge, akiutangaza mji wa PyeongchangPicha: picture alliance/dpa

Mji wa Pyeongchang, umeshinda zabuni kwa kauli mbiu ya "upeo wa fikra mpya'', baada ya kupata ushindi wa kura nyingi dhidi ya miji mingine iliyokuwa ikiigombea nafasi hiyo, Munich wa Ujerumani na mji wa Annecy wa Ufaransa, kutoka katika kamati ya Kimataifa ya Olympic.

Südkorea Olympische Spiele Pyeongchang 2018
Rais wa Korea ya Kusini Lee Myung-bak (katikati) akisherehekea pamoja na wajumbe wenginePicha: picture alliance/dpa

Awali akizungumzia ushindi huo wa Korea kusini, Rais wa kamati ya Kimataifa ya Olympic Jacques Rogge amesema ushindi huo mkubwa uliopata mji wa Pyeongchang, katika awamu ya kwanza ya uchaguzi, umemshangaza hata yeye binafsi.