Mjadala wazuka kuhusu usalama wa majukwaa ya kuchimbia mafuta. | Matukio ya Kisiasa | DW | 24.06.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mjadala wazuka kuhusu usalama wa majukwaa ya kuchimbia mafuta.

Maafa ya kumwagika mafuta katika eneo la ghuba ya Mexico yaliyosambaa hadi katika maeneo mengine nchini Marekani ni suala linaloushughulisha pia umoja wa Ulaya kuhusu usalama wa kuchimba mafuta .

default

Moja kati ya majukwaa kadha ya kuchimbia mafuta baharini katika ghuba ya Mexico nchini Marekani.

Maafa ya kumwagika kwa mafuta katika eneo la ghuba ya Mexico yaliyosambaa hadi katika maeneo mengine nchini Marekani, ni suala ambalo limewashughulisha wengi hadi katika bara la Ulaya kuhusu usalama wa majukwaa ya kuchimbia mafuta baharini. Kundi la vyama vya ulinzi wa mazingira, The Greens katika bunge la Ulaya na mashirika kadha ya ulinzi wa mazingira yanataka kuwepo na usalama wa hali ya juu, wakati halamashauri ya umoja wa Ulaya inadai kuchukuliwa hatua za tahadhari zaidi dhidi ya makampuni makubwa ya mafuta.

Majukwaa 400 yako katika eneo la bahari ya kaskazini, inasema halmashauri ya umoja wa Ulaya. Umri wa majukwaa hayo kwa wastani ni miaka 17, kwa tathmini iliyotolewa na vyama vya ulinzi wa mazingira katika bunge la umoja wa Ulaya. Gabriella Zanzaniane kutoka katika shirika la ulinzi wa mazingira, Food and Water Watch anasema.

Iwapo hata makampuni yenyewe ya mafuta yameyaweka majukwaa yao ya kuchimbia mafuta kuwa yana hatari, ni makosa kudai kuwa katika bara la Ulaya hakuna hatari. Pamoja na hayo , iwapo kuna matatizo na makampuni ya mafuta, matatizo hayo pia yapo katika uchimbaji wa mafuta chini ya bahari.

Kamishna wa nishati katika umoja wa Ulaya Günter Oettinger lakini ana matumaini ya nia njema kutoka kwa makapuni ya mafuta. Kanuni pekee haziwezi kuleta hali ya usalama kwa asilimia 100, amefafanua hayo Oettinger. Mengi yanategemea mtazamo na utendaji wa makampuni hayo. Ndio sababu Oettinger ameyataka makapuni hayo kutoa maoni yao.

Tumetayarisha maswali yanayogusa sehemu zote, kuhusiana na hatua za usalama za tahadhari, lakini pia sera za udhibiti kuhusiana na uwezekano wa hatari ya uharibifu kutokea, kuhusu ufundi, na maswali yote ya kisheria.

Oettinger amesema kuwa jibu litapatikana wakati wa mkutano utakaofanyika mwezi Julai. Iwapo itakuwa muhimu sana atatoa mapendekezo majira ya mapukutiko ya umoja wa Ulaya.

Sandy Luk, , mtaalamu wa masuala ya sheria kutoka shirika la mteja dunia, "Client Earth", anaona kuwa kuna umuhimu mkubwa, anapoangalia sheria na maelekezo ya kimataifa na yale ya umoja wa Ulaya.

Majukwaa ya kuchimbia mafuta hayapaswi kufungwa, inasema mwanasheria huyo kutoka shirika hilo la Client Earth. Na makampuni ya mafuta binafsi yanafanya uzembe katika kulinda usalama, vinasema vyama vya ulinzi wa mazingira, The Greens katika bunge la Ulaya. Euro bilioni 39 zimewekezwa na makampuni hayo katika utafutaji wa sehemu nyingine zenye mafuta na kiasi cha euro milioni 20 tu katika utafiti wa masuala ya kiusalama.

Mwandishi : Andreas Reuter / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri:Mtullya abdu

 • Tarehe 24.06.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/O2Q0
 • Tarehe 24.06.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/O2Q0

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com