Mivutano ya Tchad na Sudan yakorofisha juhudi za amani Darfour | Habari za Ulimwengu | DW | 09.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mivutano ya Tchad na Sudan yakorofisha juhudi za amani Darfour

New-York

Afisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa ametahadharisha dhidi ya kuzidi makali mvutano katika jimbo la Darfour,pamoja na ugonvi kati ya Tchad na Sudan,akisema hali kama hiyo itakorofisha juhudi za amani za kimataifa."Hali katika jimbo la Darfour imezidi kua mbaya kutokana na matumizi ya nguvu ya hivi karibuni nchini Tchad"-amesema hayo naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa anaeshughulikia opereshini za kulinda amani,Jean Marie Guéhenno mbele ya baraza la usalama la umoja wa mataifa.Mwanadiplomasia huyo wa kutoka Ufaransa alikua ziarani hivi karibuni katika jimbo la machafuko la Darfour.Jean Marie Guéhenno amezilaumu serikali za Tchad na Sudan akisema mitindo ya kulaumiana kati yao inazidi kupalilia mizozo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com