Mission Berlin – Mada | Mission Europe | DW | 05.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mission Europe

Mission Berlin – Mada

Jukumu la Anna ni kuwazuia majambazi wa wakati wasirejeshe saa nyuma na kuisababishia Ujerumani ghasia za kihistoria.

Anna ndiye mhusika mkuu katika Mission Berlin

Anna ndiye mhusika mkuu katika Mission Berlin

Anna yuko mkahawani, Berlin. Mwanamke fulani ameuawa katika chumba nambari 40. Anna anatuhumiwa kuwa amehusika kwenye mauaji hayo.

Kachero anakuja kumhoji na anapata ujumbe wa kushangaza umeandikwa kwa lugha ya kijerumani kwenye kioo cha bafu: "In der Teilung liegt die Lösung. Folge der Musik." ("Suluhu iko kwenye mgawanyiko. Fuata muziki")

Je ujumbe huu una maana gani? Je huenda ujumbe huo unalenga kasha la zamani la muziki lililo juu ya dawati? Je Anna ataweza kutengua kitendawili hicho?

Kwa kuwa Anna ni mhusika halisi kwenye mchezo wa kompyuta (tarakilishi), anasaidiwa na mchezaji. Mchezaji anashughulika kwenye kompyuta yake na anamwongoza Anna kupitia Berlin na pia kuzingatia wakati -- tangu Berlin Mashariki hata Berlin Magharibi na pia kutoka mwaka 2006 kurudi mwaka 1961 kisha kurejea mwaka muhimu wa 1989.

Mchezaji anachanganua hali pamoja na Anna, lakini mwishowe anatakiwa kutoa uamuzi ambao huenda ukamtatiza Anna.

Viungo vya WWW