Mission Berlin 12 – Muziki wa Kanisa | Mission Berlin - Episoden | DW | 20.03.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Mission Berlin - Episoden

Mission Berlin 12 – Muziki wa Kanisa

Anna amebakiwa na dakika 65. Anatambua kuwa kikasha cha muziki ndicho sehemu inayokosekana kwenye kinanda cha kanisa. Mwanamke mwenye mavazi mekundu anajitokeza na kudai apewe ufunguo. Ufunguo gani?

Kinanda cha kanisa la Gethsemane kina siri gani?

Mission Europe / Mission Berlin / Episode 12

Anna anasikia wimbo anaoufahamu. Kinanda cha kanisa kinatoa mirindimo sawa na ile ya kwenye kikasha cha muziki. Wakati Anna anapokikaribia kinanda anamsikia mtunza kanisa akimweleza mgeni kuwa kinanda hicho kimerekebishwa ila kinakosa kipande kimoja…ein Element.. tangu ukuta ulipojengwa. Anna anatambua kuwa kikasha ndicho kiungo kinachokosekana na anakibandika kwenye kinanda. Kinanda kinapoanza kupiga, mlango unafunguliwa na anajikuta akiwa amekabiliana na mwanamke mwenye mavazi mekundu. Anatokwa na uhai mwingine na anasaliwa na dakika 60 pekee.

DW inapendekeza

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa