1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri ni mabingwa tena wa Afrika

11 Februari 2008

Misri iliikomea jana Kamerun bao 1:0 na kutwaa kombe la Afrika hadi cairo kwa mara ya 6.

https://p.dw.com/p/D5mN

Maalfu ya wamisri-wake kwa waume wakubwa kwa wadogo walimiminika jana usiku mitaani mjini cairo,wakipepea bendera zao na wakiimba kushangiria ushindi wao wa 6 wa kombe la Afrika la mataifa huko Accra,Ghana baada ya Misri kuwazaba simba wa nyika bao 1:0.

Mabingwa Misri wamechangia mastadi 5 katika timu bora kabisa ya wachezaji stadi 11 wa kombe hili la 2008-wakijumuisha kipa wao El-Hasdary,mtiaji bao la ushuindi Aboutraika pamoja na mshambulizi Amr Zaky.

Na je, kombe la Afrika 2008 lililojionea jumla ya mabao 99 ndilo lilionesha ustadi wa juu kabisa wa dimba la Afrika kuliko yote tangu Khartoum,1957 lilipoanzishwa?

Hayo pamoja na mapya kutoka bundesliga na premier League,ndio niliowaandalia jioni hii.

Tuanze na Kombe la Afrika la mataifa lililoanza Januari 20 mjini Accra na kumalizika jana mjini humo kwa ushindi wapili mfululizo wa Misri baada ya kuikandika kamerun bao 1:0 kutokana na madhambi ya nahodha wao Rigobert Song:

Nahodha wa simba wa nyika-kamerun Rigobert song,alifanya jana madhambi makubwa langoni mwake na Mohamed Zidan,akamuadhibu kwa kumpokonya dimba na kumtupia mpira mwenzake Abou Trika kutia bao pekee na la ushindi n a taji la sita la mafiraouni.

Kwa ushindi huo wapili mfululizo, maalfu ya wamisri ,wake kwa waume,wakubwa kwa wadogo wakamiminika usiku wa jana katika barabara na mitaani mjini cairo na jirani Giza kuanza shangwe na shamra-shamra.Ilikua asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu alitia gongo:

Mkutano na nje.mashabiki walikumbatiana na kupaza sauti „MASRI,MASRI“ huku magari yakihanikiza kwa vin’gora na kulemaza misafara yote majiani.

„mafiraouni ni wafalme wa Afrika“- ndio kichwa cha maneno katika mtandao wa michezo maarufu nchini misri wa www.Filgoal.com.

Vituo vya Tv nchini Misri vilipiga nyimbo za kuadhimisha ushindi wa jana na kuwapongeza mastadi wao na kocha wao hassan Shehata alieiongoza timu kutwaa pia kombe hili miaka 2 nyuma 20006 nyumbani Cairo.

Shujaa wa jana lakini alikua tena Mohamed Aboutrika,mchezaji maarufu kabisa nchini Misri alietia pia lile balo la ushindi la mwakaju wa mwisho wa penalty 2006 lililoinyima kombe Ivory Coast.

Shabiki mwengine alidai lakini, „sifa zote ziende kwa Hassan Shehata,kwani haya ni mafanikio makubwa sana kwake yeye.Shehata aliegemea zaidi mastadi wanaocheza dimba nyumbani Misri na licha kuwa walikata tiketi yao ya Ghana wakiyumbayumba, Misri iliwakosoa mabingwa wengi kwa jinsi ilivyotamba nchini Ghana.

Hii ni mara ya 3 tu kwa mabingwa watetezi kufaulu kulitwaa tena kombe la Afrika katika historia ya kombe hili.Misri ilikuwa ya kwanza kufanya hivyo, ilipolitwaa Khartoum, 1957 na utamu ulipoikolea ikalitwaa tena nyumbani cairo,1959.Sasa baada ya kutamba nyumbani 2006 imetamba tena Accra,2008.

Simba wa nyika –kameroun ni timu ya pili kuiigiza Misri kwa kulitwaa kombe mara 2 mfululizo.

Kameroun ilitamba 2000 na ikiwa njiani kuelekea kombe la dunia 2002 huko Korea ya kusini ikatoroka nalo tena hadi Yaounde.

Misri ilioiwalaza simba wa nyika hapo kabla katika kombe hili Januari 22 mjini Kumasi kwa mabao 4:2,ilijipatia nafasi nyingi za kuona mlango wa Kamerun ma mapema,lakini kipa wa Kamerun Idriss Kameni akiokoa maridadi ajabu.

Mkakati wa simba wa nyika ,ulikua kuwanasa mafirauni kwa mtego wa kurudisha hujuma za ghafula-counter-attack-lakini walishindwa kumlishia mpira mshambulizi wao Samuel Eto’o ambae alikua hatari kabisa katika lango la Misri dakika 10 kabla ya kipindi cha mapumziko.

Baada ya kamerun kufumaniwa na bao la Abou Trika mnamo dakika ya 77 ya mchezo,Kamerun ilichhachamaa kidogo na mara mbili ilimtia shindo kipa stadi wa Misri, Essam Al Hadari aliokoa maridadi kabisa.Nahodha Rigobert Song alielizasmisha jahazi lake,nusura aliokoe kuzama pale alipotia mpira kicha na kupita juu kidogo ya lango la Misri sekunde chache kabla ya firimbi ya mwisho kulia.

Mwishoe, mlinzi wa simba wa nyika-Geremi akifuta machozi

Alielezea hisia za wakamerun wote aliposema,

„Hatupendi kushindwa na hasa katika finali,lakini habari nzuri kabisa ni kwamba tulicheza finali,kwani watu wengi hawakudhani tungefika hapo.“

Hebu sasa tuchambue jinsi kombe hili la 26 lilivyokwenda na tumepata maarifa gani:

Inakubaliwa na mabi ngwa wote wa dimba kuwa kombe la 26 la afrika sio tu limesusimua kuliko yote hadi sasa na ufundi wa dimba wa timu za Afrika umeongezeka,lakini kumebainika pia kasoro katika uwezo wa bara la Afrika kimaandalio:

Afrika iliwatembeza mastadi zaidi wa dimba walioonekana dunia nzima mnamo wiki 3 zilizopita.Tumeona mchezo wa kushambulia na idadi ya magoli 99 katika mechi 32 ni ushahidi wa hayo.

Upande wa mastadi,mabingwa Misri licha ya kuwa inaegemea zaidi wachezaji wa nyumbani kutoka klabu zake 2 Al Ahly na Zamalek, imechangia wachezaji 5 katika listi ya timu bora ya Afrika kutoka kombe hili:

Wakati samuel Eto’o wa Kamerun ameibuka mtiaji mabao mengi kuliko yeyote-mabao 5 na kuivunja ile rekodi ya Muivory Coast-Laurent Pokou ya mabao 14 kwa kuweka rekodi mpya ya mabao 16,Misri inajivunia mastadi wake 5 katika timu bora ya Afrika Cup 2008: Kipa wao Essam al-Hadaray,beki wao mshahara Wael goma,wachezaji wake wa kiungo-Mohamed Aboutraika na Hosny Abd Rabou na bila shaka msham,bulizi aliepachika mabao 4 Amr zaky.

Makamo-bingwa kamerun wamechangia mastadi 2-mlinzi Geremi Njitap na mchezaji wake wa kiungo Alexandere Song.hata Angola imechangia alao stadi mmoja katika kikosi hicho bora cha Afrika:Mshambulizi wao manucho anaeelekea msimu huu Manchester united.

Tembo wa Ivory Coast waliopigiwa upatu sana kutoroka na kombe hili,baada ya kuteleza mbele ya Misri na halafu kupokonywa nafasi ya 3 na wenyeji Ghana hapo jumamosi, wam etoa stadi mmoja tu katika Listi hiyo:mchezaji wao wa kiungo yaya Toure.

Wenyeji Ghana kwa msangao wa wengi,imetia stadi mmoja lakini katika safu ya walinzi:mchezaji wao wa kiungo Michael Essien,aliejaza pengo la nahodha John Mensah,aliefungiwa kucheza pale Ghana ilipokutana na Kamerun katika nusu-finali.Ghana imetoa pia stadi mwengine –nae ni Sulley Muntari.

Kilichokwenda kombo na kukosolewa mno katika kombe hili la 26 la Afrika nchini Ghana ni maandalio pamoja na kasoro kadhaa zilizoonekana:

Mechi nyingi zilichezwa katika viwanja nusu-vitupu na waandazi walishindwa kuwatia shime mashabiki wa nyumbani kujaza viwanja.Au tiketi zilikua za bei ya juu ?

Kwani hata finali ya jana ilipita bila uwanja kusheheni kamili.

Viwanja -2 kati ya hivyo vikiwa vimejengwa kisasa kabisa na machina, zana nje ya viwanja hivyo hazikuridhisha.

Labda iliofedhehesha zaidi ni pale kocha wa timu mwenyeji-Ghana-mfaransa Claude Le Roy alipokosoa hadharani hali ya uwanja mkuu Accra.Alinukuliwa kusema,

„Mnamo miaka 20 ya kuwapo Afrika ,ni uwanja mbovu kabisa niliojionea.“

Kuhusu mahoteli imeonekana kwa mfano wachezaji wa bafana Bafana wakiongozwa na kocha wao mbrazil,carlos Parreira, wamezowea kupiga kambi katika hoteli za kifahari,lakini waliwekwa katika Hoteli ya daraja ya 2-star huko Tamale ambako mbuzi wakitembea bila pingamizi nje tu ya hoteli hiyo.

Halafu lile jaribio la hongo:Timu 2-Benin na namibia zilidai kwamba ziliendewa na mtu asiejulikana kuzihonga fedha ili kufanya mizengwe katika mechi zao.CAF-shirikisho la dimba la Afrika likaahidi kukichunguza kisa hicho.

Afrika kusini ikiwa ni mwenyeji wa kombe lijalo la dunia 2010 yafaa kutega sikio.Claude leroy ametoa ushauri huu,

„Jambo la kwanza kabisa sio kuweka viti maridadi vya kupumzikia watu mashuhuri katika ukumbi wa VIP, bali ni kuona uwanja wa dimba ni safi kabisa.“

Baada ya kombe la Afrika nchini Ghana ,timu zinarudi nyumbani kujiwinda na changamoto za kuania tiketi kwa kombe la dunia 2010 huko Afrika kusini.Tanzania ina miadi na simba wa nyika –kamerun .swali kwa watanzania ,je, simba akiroa maji kama ilivyoonekana jana mjini Accra,msimuogope:Gwiji mashuhuri la dimba la Tanzania Dokta Liki Abdullah laonya Taifa Stars,wasifanye dharau hiyo:

Katika kinyan’ganyiro cha Ligi mashuhuri barani Ulaya:

Katika Bundesliga,Werder bremen ilizima vishindo vya viongozi wa ligi Bayern munich nyumbani mwao ilipomudu kutoka suluhu bao 1:1 katika allianz arena hapo jana.Laiti Munich ingeshinda,ingelifungua mwanya wa pointi 6 kutoka Bremen.

Diego alilifumania kwanza lango la Munich na licha ya kupata mkwaju wa penalty kusawazisha, ilikosa kutia bao.Mwishoe, Ze Robert aliokmoa Munich kwa bao lake.

Je,kutoka jana suluhu na Bremen ilistahiki na haki ?Meneja wa Bayern munich Uli Höenes anabisha:

„La,hasha,haikua haki kutoka sare,kwani Bremen imevuka tu chupuchupu kushindwa.“

Alidai meneja wa Bayern Munich.

Katika mpambano mwengine wa kusisimua jana, Schalke iliwalaza mahasimu wao wa mtaani Borussia Dortmund mabao 2:1.munich inaongoza Bundesliga sasa kwa pointi 4.

Katika Premier League-ligi ya uingereza,Manchester united ilistushwa na pigo kutoka kwa Manchester City l mabao 2-1

Hatahivyo, Manchester yadai mbio za kuatawazwa mabingwa msimu huu hazikumalizikia hapo.