Mishahara ya mawaziri na wabunge | Magazetini | DW | 22.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Mishahara ya mawaziri na wabunge

Serikali yabatilisha uamuzi wa kujiongezea mishahara

Kansela Angela Merkel bungeni mjini Berlin

Kansela Angela Merkel bungeni mjini Berlin


Licha ya mapumziko ,baadhi ya magazeti yamechapishwa humu nchini na kuzingatia mijadala kuhusu nani atetee wadhifa wa rais wa shirikisho baada ya mhula wa rais wa sasa kumalizika.Uamuzi wa serikali ya shirikisho wa kuachana na mpango wa kujipandishia mishahara nao pia umechambuliwa.


Tuanze basi na mishahara ya wabunge.Gazeti la SCHWERINER VOLKSZEITUNG linaandika:


Angela Merkel hakupoteza wakati.Kiongozi huyo wa serikali na mawaziri wake walitambua,ghadhabu za umma zingemuangukia yeye tuu.Hata kama mishahara ya mawaziri haikuongezeka tangu miaka kadhaa iliyopita.Leo hivi kesho hivi,kile kinachostahiki kupiganiwa ,kufumba na kufumbua kinabatilishwa.Kasheshe ya nyongeza ya mishahara ya wabunge na mawaziri ni ushahidi wa kusikitisha wa dosari iliyopo katika uongozi na ukosefu wa moyo wa kisiasa.Kwamba siku za mbele mshahara wa waziri hautatofautiana sana na ule wa afisa wa ngazi ya juu serikalini,suala hilo limewekwa kando kama ulivyodharauliwa ukweli kwamba wasomi hawatapendelea tena kujijenga kisiasa ikiwa mishahara haitakua ya kuvutia.


Hayo ni maoni ya SCHWERINER VOLKSZEITUNG.Kwa upande wake gazeti la LAUSITZER RUNDSCHAU linahisi:


Baraza la mawaziri limesamehe nyongeza ya mishahara.Uamuzi wa kutia moyo huo kwa wapiga kura.Baraza la mawaziri lingeweza kupita njia nyengine kabisa kurekebisha kiwango cha mishahara badala ya ile iliyotumiwa na serikali kuu ya muungano kutangaza nyongeza ya mishahara ya wabunge.Lakini hofu zimemfanya Angela Merkel aamue vyengine.Kuna sababu nyengine lakini iliyoifanya serikali iangukie mhanga wa kijicho ,nayo inatokana na ule ukweli kwamba hakuna hata mmoja nchini Ujerumani anaehisi kwamba serikali inastahiki kujiongezea hata senti moja."


Mada ya pili magazetini ni mijadala kuhusu wadhifa wa rais wa shirikisho.Gazeti la Die Welt linaandika:


Wiki kama mbili hivi zilizopita ingekua rais Horst Köhler ameonyesha ishara anapendelea kuendelea na wadhifa wake, ingetosha-hata wawakilishi wa chama cha Social Democratic katika baraza la wawakilishi wa shirikisho wangemuunga mkono kwa wingi mkubwa.Lakini kwakua hakutamka,basi fikra iliyowahi kutolewa wakati mmoja,imerejea tena midomoni:SPD wamepania kupendekeza kwa mara ya pili Gesine SCHWAN atetee wadhifa huo.Akiwa mtu mwenye fasaha zaidi kuliko Köhler,Schwan anajivunia sifa ya kuvutia makundi mbali mbali-hata yale ya mrengo wa shoto.Sifa kubwa zaid ni ile hali kwamba mfuasi huyo wa chama cha SPD alikua mkosoaji mkubwa wa chama hicho katika miaka ya 80 kwa kutozingatiwa masuala ya haki za binaadam katika siasa ya chama kuelekea nchi za Ulaya ya mashariki.


KIELER NACHRICHTEN linaonya pasije pakatokea kasheshe nyengine pindi GESINE SCHWAN akishindwa mara ya pili na Köhler.Gazeti linaendelea kuandika:


Makadirio ya uchaguzi yatazidi kuwa mabaya msimu wa mapukutiko ujao.Mkuu wa chama cha Social Democratic SPD hatoweza tena kuzuwilika hali kama hiyo ikitokea nusu mwaka tuu kabla ya uchaguzi.SPD watafanya vizuri wakimteuwa mtu mwenye nafasi nzuri ya kupigiwa kura.Hawana lakini mtu kama huyo.Na hayo pia yanazidi kukidhoofisha chama hicho.


Hatujui wahariri wa magezti watasema nini kesho,kwasababu Horst Köhler ameshatamka hivi punde atatetea kwa mara ya pili wadhifa huo.

►◄
 • Tarehe 22.05.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E4FA
 • Tarehe 22.05.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E4FA