1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miripuko zaidi Urusi

1 Aprili 2010

Umarov aungama kuamrisha hujuma ya Moscow

https://p.dw.com/p/MjwE
MOSCOW, RUSSIA.Picha: picture-alliance/ dpa

Mripuko mpya umeitikisa tena leo Urusi wakati ikizika watu kadhaa waliouwawa katika shambulio la reli ya chini ya ardhi mjini Moscow, lililofanywa na kikundi cha waislamu wenye Itikadi kali .Kikundi hicho kimeonya hujuma zaidi ziko njiani.Urusi, kwa miaka mingi sasa , ikipigana vita kukandamiza uasi wa wanamgambo wa kiislamu huko Chechnia ,Dagestan na Ingushetia.Kiongozi wa kundi hilo Umarov au" Abu Usman" , amenadi jihadi nchi nzima ya Urusi.

Hali shuari ikichafuliwa mjini Moscow na miripuko ya juzi katika reli ya chini ya aridhi,vyombo vya usalama vya Urusi, vilitikiswa tena hii leo pale gari lao linalotuiliwa shaka kusheheni miripuko liliporipuka na kuuwa watu 2 huko Dagestan. Kwa muujibu wa taarifa za mwanzo,miripuko hiyo ni ajali .Ni jana tu , pale watu 12 walipouwawa wengi wao polisi pale watu 2 walipojiripua huko Dagestan.

Urusi, kwa miaka mingi sasa, ikipigana vita na waumini wa kiislamu wenye itikadi kali katika Kaskazini mwa Caucasus, yanayodai uhuru:Chechnia,Dagestan na Ingushetia.Lakini, hujuma ya Jumatatu ni ya kwanza kuenea hadi mji mkuu Moscow tangu kupita miaka 6.

Kikundi cha waislamu kinachojiita "Emirate of the Caucasus", kinaania kuunda dola huru la kiislamu chini ya mfumo wa sharia,kilijitwika jana jukumu la hujuma mjini Moscow.

Doku Umarov, ambae amefanyiwa njama kadhaa za kuuliwa na vikosi vya usalama vya Urusi, alisema, ni yeye binafsi alietoa amri ya hujuma iliofanywa katika vituo vya reli ya chini ya ardhi mjini Moscow. Alisema na ninamnukulu,

"Kilikuwa kitendo halali cha kulipiza kisasi kwa kuendelea kuuliiwa kwa raia katika Caucasus."

Umarov, anaetumia pia jina la "Abu Usman " na ambae mwezi uliopita alinadi vita vya jihadi nchini kote Urusi,aliwaonya warusi kutarajia hujuma zaidi.Alisema ,

"Mashambulio katika ardhi ya Urusi yataendelea ili kulipiza kisasi kwa kile vikosi maalumu vya usalama vya Urusi, vinafanya katika eneo la Caucasus."

Umarov, aliongeza kusema kwamba, warusi hawatoweza tu kuangalia kwenye TV kwa starehe kinachotokea Caucasus ikiwa hawatanyanyuka kuzuwia uhalifu unaofanywa na majambazi wao chini ya uongozi wa waziri mkuu Vladmir Putin.

"Hivi ni vita vinavyokuja mitaani mwenu." alionya Umarov.Umarov, amedai hujuma zilizofanywa ni kulipiza kisasi kwa mauaji ya umma wa watu yaliofanywa na vikosi vya uvamizi vya Urusi dhidi ya wakaazi masikini wa Chechnia na Ingushetia hapo Februari 11 mwaka huu walipokuwa wakichuma vitungu thomu .

Wanazouoni wa kiislamu kutoka nchi 12 leo, wamelaani hujuma za kujiripua zilizofanywa na waasi hao wa kiislamu huko Moscow na Dagestan kuwa ni " hujuma za uhalifu wa kigaidi."

Mwandishi: Ramadhan Ali /AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman