1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miripuko yaitikisa Sri Lanka na kuuwa zaidi ya watu 160

Bruce Amani
21 Aprili 2019

Watu wapatao 160 wameuawa kutokana na mfululizo wa mabomu yaliyoripuka kwenye mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo. Polisi imethibitisha kuwa watu wengine zaidi ya 300 wamejeruhiwa

https://p.dw.com/p/3HArJ
Sri Lanka Colombo Explosion in St. Anthony Kirche
Picha: AFP/I. S. Kodikara

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Ruwan Gunasekera mlipuko mwingine umetokea muda mfupi katika hoteli iliyopo jimbo la kusini mwa Colombo la Dehiwala likiwa ni shambulio la saba kufanyika katika siku hii ya Jumapili. Mlipuko wa nane umetokea kwenye kitongoji cha Orugodawatta kaskazini mwa mji mkuu.

Mpaka sasa hakuna yeyote aliyedai kuhusika na mashambulio hayo na wala idara za usalama hazijasema iwapao mashambulo hayo yalifanywa na magaidi.

Lakini kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari mashambulio hayo yalizilenga sehemu za kidini na kiuchumi. Rais wa Sri Lanka Maithripala Sirisena amesema majeshi ya ulinzi na polisi wameanzisha uchunguzi. Viongozi mbalimbali duniani wamelaaani mashambulio hayo.