Mionzi ya nyuklia yavuja Fukushima | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.03.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mionzi ya nyuklia yavuja Fukushima

Haijulikani lini wahandisi wa Kijapani watafanikiwa kuzuia mionzi ya nyuklia inayovuja katika mtambo wa nishati ya nyuklia wa Fukushima nchini Japan. Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la nishati ya nyuklia IAEA.

In this photo released by Tokyo Electric Power Co. (TEPCO), gray smoke rises from Unit 3 of the tsunami-stricken Fukushima Dai-ichi nuclear power plant in Okumamachi, Fukushima Prefecture, Japan, Monday, March 21, 2011. Official says the TEPCO temporarily evacuated its workers from the site. At left is Unit 2 and at right is Unit 4. (Foto:Tokyo Electric Power Co./AP/dapd) EDITORIAL USE ONLY

Mtambo wa nishati ya nyuklia wa Fukushima

Maafisa wa IAEA katika makao makuu, mjini Vienna wamesema kwamba mbali na vinu nambari 1 na 2, sasa data zinaonyesha kuwa hata katika mtambo nambari 3, kuna dalili za kuvuja kwa mionzi ya nyuklia.

Afisa mkuu wa IAEA anaehusika na masuala ya usalama wa nyuklia amesema, hatua kadhaa zinahitaji kuchukuliwa hata kabla ya kuanza kutathmini kiwango cha uharibifu uliotokea.

Japan / Naoto Kan / Ministerpräsident (Foto: AP)

Waziri Mkuu wa Japan Naoto Kan

Hapo awali waziri mkuu wa Japan, Naoto Kan alisema kuwa bado kuna kazi kubwa sana ya kufanywa huko Fukushima .

Idadi ya watu waliopoteza maisha yao, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi na tsunami nchini humo tangu majuma mawili yaliyopita, sasa imefikia 10,000 na watu wengine wapatao 17,000 bado hawajulikani walipo.

 • Tarehe 26.03.2011
 • Mwandishi Martin,Prema
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RCtE
 • Tarehe 26.03.2011
 • Mwandishi Martin,Prema
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RCtE