1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MILAN : Majasusi wa CIA watakiwa mahkamani

17 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRS

Hakimu wa Italia ameamuru Wamarekani 26 na Wataliana watano kujibu mashtaka mahkamani kutokana na madai ya utekaji nyara uliofanywa na Shirika la Ujasusi la Marekani CIA mjini Milan.

Waendesha mashtaka wamesema kwamba maafisa watano wa ujasusi wa Italia walishirikiana na Wamarekani ambao takriban wote walikuwa ni mashushu wa CIA kumteka nyara sheikh wa Misri katika mtaa wa mji wa Milan hapo mwaka 2003.Sheikh huyo inadaiwa kuwa baadae alihamishwa kupitia Kambi ya Anga ya Ramstein nchini Ujerumani kwenda Misri ambapo amesema aliteswa.

Miongoni mwa wanaoshtakiwa ni pamoja na mkuu wa shughuli za ujasusi za kijeshi nchini Italia Nicolo Pollari ambaye amekanusha kufanya kosa lolote lile.

Shirika la Ujasusi la Marekani CIA limegoma kuzungumzia kadhia hiyo.