1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Migomo nchini Afrika Kusini yaendelea kwa siku ya tatu

29 Julai 2009

Kwa siku kadhaa sasa Afrika Kusini imekabwa na migomo ya wafanya kazi.

https://p.dw.com/p/Izgr
Maandamano ya wafanyakazi mjini JohannesburgPicha: picture-alliance / dpa
Wakaazi wa maeneo ya madongo poromoka katika majimbo kadhaa waliandamana kutaka huduma bora kwa umma, huku wafanya kazi wa  manispaa wakiandamana  pia kwa siku ya tatu leo wakishikilia waongezewe mishahara. Wakati huo huo, wafanya kazi katika sekta ya viwanda vya kemikali wametangaza kuumaliza mgomo wao wa siku nane baada ya kupewa nyongeza ya mishahara baina ya asilimia tisa na kumi. Uchumi wa Afrika Kusini unajionea kwenda chini sana kuwahi kuonekana tangu mwaka  1992, na vyama vya wafanya kazi vinasema hali hiyo inawaumiza sana walio maskini. Othman Miraji alimuuliza kwa njia ya simu mwandishi wa habari Issac Khomu juu ya mgomo wa wafanyakazi wa manispaa, unaendelea vipi? Mwandishi: Othman Miraji Mhariri: Mohamed Abdulrahman