Michezo:Africa Cup | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 22.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Michezo:Africa Cup

Ivory Coast,Morocco na Mali ziliondoka jana na pointi 3 kila moja katika kinyan'ganyiro cha kombe la 26 la Afrika.

Katika siku ya pili ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Ghana Salomon Kalou jana aliichenga ngome nzima ya Nigeria tena maridadi-ajabu na kuipatia Ivory Coast bao la ushindi dhidi ya „super eagles“-Nigeria .

Morocco na Mali pia ziliondoka na ushindi.Morocco ilivunja tumbuu ya lango la Namibnia dakika ya kwanza ya mchezo na mwishoe, ikaiifunza Namibia darasa la mabnao 5-1 lao.Soufiane Alloudi wa Morocco, pekee alipachika mabao 3 –hattrick.

Jogoo la sevilla- Freddie Kanoute yeye alitosheka na bao la penalty kuipiga kumbo Benin iliochachama hadi firimbi ya mwisho.

Nigeria inarudi uwanjani ijumaa hii kuamua hatima yake na ya kocha wao mjerumani Berti Vogts ikiwa na miadi na Mali wakati Tembo wa Ivory Coast, wamepanga pointi 3 nyengine kutoka Benin siku hiyo hiyo.

Corte d’Iviore au Ivory Coast haikuvunja moyo mashabiki wake walioipigia upatu kwamba ni timu itakayotoroka na kombe hapo februari 10.Ilikua lakini Nigeria,iliokaribia kutangulia kutia bao pale mkwaju wao ulipogonga mwamba.Lakini ilikua stadi wa Chelsea Salomon Kalou aliewachenga walinzi wa Nigeria kistadi kabisa na baadae akafyatua mkwaju ulionasa katika wavu wa Super Eagle. Kocha wa Ivory Coast aliechukua mikoba wiki 2 nyuma kutoka kocha mjerumani Uli Stiliecke,Gerard Gili,baadae alisema, „ulikua mwanzo mwema.Wachezaji wangu walitamba kweli.Tuendelee namna vile.“

Nae kocha wa Nigeria-mjerumani Berti Vogts,alifungua kitabu cha historia ya dimba kujieleza msiba uliowapata jana „super eagles“.Tulishindwa mechi ya kwanza katika kombe la Afrika 2006 na baadae tukaingia duru ya pili,lakini dhidi ya Mali mpambano ujao itatupasa kucheza bora zaid ijumaa ijayo.“-alisema Berti Vogts.

Pale corte d’Iviore ilipoibuka makamo-bingwa mjini Cairo miaka 2 nyuma, mfaransa Henri Michel alikuwa ndie kocha wao.jana Michel aliwaongoza simba wa Atlas-Morocco msituni kuwatafuna chipukizi wa Namibia ambao hii ni mara ya pili tangu 1998 wanacheza katika Kombe la Afrika la mataifa.

Matokeo yake simba wa Atlas walinguruma kwa vishindo tena kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho.

Firimbi ya mwisho ilipolia,chipukizi wa Namibia kikapu chao kilijaa mabao 5 kwa moja lao.Morocco ambayo ilipigwa kumbo duru ya kwanza tu ya kombe lililopita nchini Misri 2006,licha ya kuwa makamo-bingwa 2004 nchini Tunisia,imetertemsha timu changa kabisa inayoonana kwa pasio za kasi na maridadi.Jogoo lao ni chipukizi aitwae Souffiane Alloudi alietia mabao 3 pekee katika kimia cha Namibia.Kwa bahati mbaya,yaonesha huenda hayo yakawa mabao yake ya mwisho katika kombe hili,kwani Alloudi ameumia.

Changamoto ya 3 jana ilikua kati ya Mali na Benin.Mali ilihitaji mkwaju wa penalty wa stadi wao Freddie Kanoute kuvunja ubishi wa Benin.

Leo ni zamu ya mabingwa na mafiraouni Misri kuoneshana na simba wa nyika –Kamerun kile kilichomtoa kanga manyoya mjini Kumasi kabla mabingwa wa Challenge cup-Sudan kukwepa risasi kali za Chipolopolo –Zambia .

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com