Michezo ya redio kuhusu uhalifu na vijana Afrika | Karandinga | DW | 21.02.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Karandinga

Michezo ya redio kuhusu uhalifu na vijana Afrika

Ungana na wapelelezi wetu wanaopambana kutafuta ukweli na haki kuhusu masuala muhimu.

Mchezo wa Karandinga unaendelea.

Wapambanaji dhidi ya uhalifu: Visa vipya vya kusisimua–wasiwasi zaidi na burudani, vikisindikizwa na elimu yenye manufaa. Ungana na wapelelezi wetu wanaopambana kutafuta ukweli na haki kuhusu masuala muhimu. Uhalifu wa mitandao, unyanyasaji wa majumbani, rushwa, uchafuzi wa mazingira, biashara haramu ya watu, ugaidi, uwindaji haramu, unyakuzi wa ardhi na dawa za bandia.

Huu wote ni mfululizo wa hadhithi zetu kuhusu changamoto zinazowakabili vijana wa Afrika. Katika kuendelaza utamaduni wa Noa Bongo, Jenga Maisha Yako, ambao ni mfululizo wenye mafanikio wa michezo ya redio, simulizi za Karandinga zinatoa taarifa muhimu na kuwahamasisha wasikilizaji kutafuta suluhisho wenyewe ili kuchukua hatua za maana katika mfumo wa burudani.

Michezo hiyo ya redio inaandikwa na waandishi wa Kiafrika na kuigizwa na wasanii kutoka kote barani. Kila moja ya hadithi simulizi hizo tatu ina vipindi 10 vyenye urefu wa dakika 12 kila kimoja.

Kipindi hicho kinapatikana kwa lugha za Kiingereza, Kifaransa, Hausa na Kiswahili. Michezo ya Karandinga inatangazwa na DW na vile vile kupitia redio washirika zaidi ya 400 kote barani Afrika. Maudhui yote yanapatikana mtandaoni kupitia dw.com/karandinga na pia inawekwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii ya DW.