1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo ya Jumuiya ya Madola yafikia tamati

4 Agosti 2014

Mji wa Glasgow umesherehekea kumalizika kwa Michezo ya Jumuiya ya Madola katika tamasha la kipekee, huku waandalizi wakiwapongeza washiriki kwa kile walichokiita kuwa ni “Michezo ya Kirafiki”.

https://p.dw.com/p/1Cof3
Commonwealth Games/ Glasgow
Picha: Reuters

Wanariadha 4,700 kutoka nchi 71 sasa wanaelekea makwao baada ya kushiriki katika michezo hiyo iliyodumu siku 11.

Bendera ya Michezo ya Jumuiya ya Madola ilikabidhiwa maafisa wa Australia ambao ndio watakaoandaa michezo ijayo mwaka wa 2018, katika mji wa Gold Coast, wa jimbo la kaskazini mashariki la Queensland.

Na hata wakati ikikabidhiwa bendera, Australia iliondolewa kileleni mwa msimamo wa medali kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1986. England ilinyakua nafasi ya kwanza ikiwa na dhahabu 58, ikifuatwa na Australia katika nafasi ya pili na dhahabu 49. Canada ilikuwa ya tatu na 32 wakati Scotland ikimaliza ya nne na 19.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Rueters/APE
Mhariri: Mohammed Khelef