Michezo wiki hii | Michezo | DW | 20.02.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo wiki hii

Hertha Berlin na Wolfsburg katika Bndesliga

Andrej Woronin (r) Hertha BSC Berlin

Andrej Woronin (r) Hertha BSC Berlin

Katika Bundesliga,je,Hertha Berlin ikiwa uwanjani wakati huu itamudu mwishoe kubakia kileleni leo ikiwa na miadi na wolfsburg ambayo mapambano 11 mfululizo haikushindwa-wauliza mashabiki ?

-Mabingwa Bayern Munich, baada ya kupoteza pointi kwa Berlin jumamosi iliopita, hawadiriki kupoteza poingti nyengine nyumbani wakicheza na stadi wao Podolski dhidi ya FC Cologne.

-Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, adai "Chelsea msimu huu wasahau taji",

-kinyanganyiro ni kati ya Manu na Liverpool.

Hertha Berlin imerudi kwa mara ya kwanza kileleni mwa Bundesliga tangu 2006-shukurani kwa mabao 2 maridadi ya Muukrain, Andrey Voronin, ambae baada ya hodi hodi nyingi,alilifumania lango la Bayern Munich mara mbili na kukaribishwa ndani.

Kombe la Dunia 2010 la kwanza barani Afrika ,linanyemelea na kwa muujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya maandalio ya Kombe hilo Danny Jordaan,tiketi zake tayari ziko masokoni. Bei za tiketi ukilinganisha na ilivyokua Ujerumani wakati wa kombe la 2006 au kwengineko miaka ya nyuma si za juu hivyo na kila shabiki aweza kumudu.Tiketi ya chini kabisa ni kiasi cha dala 20-sawa na Rand 50 za a Afrika kusini. Swali ni iwapo kweli kila mmoja aweza kumdu bei hiyo au viwanja vingi vitakuwa vitupu ?

Kulikuwapo na hofu muda mrefu kwamba, mashabiki barani Afrika watashindwa kwenda viwanjani kwa wingi ingawa wakati wa matembezi yake mara iliopita huko Afrika kusini kukagua viwanja, rais wa FIFA, Sepp Blatter,aliwaahidi wafanyi kazi wote wa ujenzi tiketi za bure.

Wengine wanajiuliza:waweza kuagiza tiketi hizo kupitia mtandao wa internet kama ilivyofanyika hapa Ujerumani ?

Lakini,Juni 14 hadi 28-yaani miezi 3 kutoka sasa, Afrika Kusini itaandaa lile Kombe la mashirikisho-Confederations Cup linalo wapambanisha mabingwa wa mashirikisho ya kanda zote za FIFA. Afrika itawakilishwa na timu 2 mara hii:mabingwa Misri na wenyeji Bafana Bafana(Afrika Kusini).

Mbali na timu hizo 2 za Afrika, kuna mabingwa wa dunia-Itali,mabingwa wa ulaya Spain,Iraq -ikiwakilisha Asia na New Zealand eneo la CONCACAF. Marekani ni mabingwa wa Amerika ya kaskazini.

Kwavile kinyanganyiro hiki ni cha kufungua pazia la kombe la dunia mwakani 2010,ulimwengu utaangalia sio tu maandalio yamefika wapi bali pia iwapo shetani wa Kombe la dunia la kwanza barani Afrika ameshaanza kupunguwa na wachawi na wapiga-ramli wameshaanza finali yao ya kuamua wapi Kombe 2010 litaelekea.

Baada ya kumalizika Kombe hilo la mashirikisho -Confederations Cup hapo Juni yatafuata mashindano yapili kwa ukubwa mwaka huu August 20 mjini Berlin: mashindano ya ubingwa wa riadha ulimwenguni-yapili katika ardhi ya Ujerumani tangu yale ya 1993 :