Michezo wiki hii | Michezo | DW | 04.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo wiki hii

Spian kujipatia kocha mpya wa taifa wa dimba.Miruz Yifter awaandaa waethiopia kwa Olimpik.

Taji la ubingwa wa Tennis la Wimbledon,linaenda kwa mmoja kati ya dada 2 wa williams-Venus au Serena.

Wanariadha wa Afrika pamoja na wale wa kenya wakijiandaa kwa michezo ijayo ya olimpik,tunawasimulia juu ya mmoja kati ya mabingwa wakubwa wa Ethiopia wa masafa marefu-mzee Mirus Yifter.

Kocha wa zamani wa Real Madrid, del Bosque yamkini sana kwa muujibu shirikisho la dimba la mabingwa wa Ulaya Spian akajaza pengo lililoachwa na mzee Luis Aragones, alieiongoza Spian jumapili iliopita kutwaa kombe la Ulaya la mataifa.

Hayo na mengineo, ndio niliowaandalia katika ulimwengu wa michezo wiki hii:

Tuanze na dimba:

Vyombo vya habari nchini Spian, vimeripoti kwamba Del Bosque,alieiongoza klabu ya Real mara 2 kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya-champions league na mara mbili taji la Spian,tayari ameridhiana kwa mdomo na shirikisho la Spian na huenda akafunga mkataba mnamo wiki 2 zijazo.

Mzee Aragones,atakaefikia umri wa miaka 7o baade mwezi huu,alijiuzulu baada ya ushindi wa kombe la ulaya -taji lao la kwanza tangu kupita miaka 44.Alisema kwamba shirikisho la dimba la Spain,halikumuomba aendelee.Aragones akafunga safari juzi alhamisi kwenda Istanbul kufunga mkataba wa miaka 2 na Fenerbahce,klabu maarufu ya Uturuki.

Wakati Spain inachagua kocha mpya, Ufaransa inadai "usiache mbachao kwa msala upitao".Inasalia na kocha wake yule yule wa zamani:

Raymond Domenech,anabakia kocha wa Ufaransa ili kuiongoza hadi kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini.Hii licha ya kupigwa kumbo Ufaransa na mapema nje ya kombe la ulaya.Dominique alikosolewa mno kwa hilo na hasa kwa kuondokea na bao 1 na point 1 tu kutoka kombe la ulaya.

Domenech aliungwamkono asalie kitini na nahodha Patrick Vieira,rais wa UEFA Michel Platini na stadi Franck Ribbery stadi wa Bayern Munich, mabingwa wa Ujerumani.

Miongoni waliochoka na Dominique, ni nahodha wa zamani Zinedine Zidane.Wao walimpendekeza nahodha wa zamani wa Ufaransa, Didier Deschamps.

Mwishoni mwa wiki hii, ama Serena au venus Williams anatawazwa bingwa wa wimbledon.Hii ni changamoto kubwa kati ya dada wawili -waamerika weusi.Wote wawili walikata tiketi zao za finali hii na watagawana pia kitita kikubwa cha fedha. Upande wa wanaume yaonesha ROger Federer wa uswisi atatoroka na taji lake la 6.

Michezo ya olimpik ya Beijing ikinyemelea, hapo August 8,rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa,atahudhuria ufunguzi wa michezo hiyo ya Beijing.Awali Sarkozy, alitishia kutohudhuria kutokana na mkomoto wa polisi wa China huko Tibet.

Kwa muujibu wa uchunguzi wa maoni kupitia mtandao, kiasi cha 90% ya wa wachina, wanapinga kuhudhuria kwa rais huyo wa Ufaransa michezo ya Beijing hapo august 8.Hii ni kutokana na msimamo wake mkali na wa kiadui aliouchukua dhidi ya China wakati wa machafuko ya Tibet.

Wanariadha wa afrika mashariki na hasa Kenya na ethiopia wamo kujinoa kwa michezo ijayo ya Olimpik.Kenya tangu mwisho wa wiki iliopita imekuwa na changamoto za kuwatafuta mabingwa na kivumbi hicho kiliendelea hadi jana Julai 4.

Mahasimu wakubwa wa Kenya huko Beijing katika mbio za masafa ya kati na marefu kuanzia mita 800 hadi marathon, watakuwa majirani zao Ethiopia:

Miongoni mwa majina makubwa ya waethiopia leo ni Kenenisa Bekele anaefuata nyayo za mzee haile Gebreselassie.

Lakini kabla selassie,alitamba mzee Miruzs Yifter,bingwa wa olimpik wa mita 5000 na 10.000 katika michezo ya Olimpik ya mosco,1980.yeye alifuata tu nyayo za marehemu Abebe Bikila na mamo Wolde.

Mzee Yifter leo anasaidia kuwafunza mabingwa wa changa wa ethiopia ili waseleleze mila ya Bikila aliekipingia miguu chini mjini Roma, 1960 na kutwaa medali ya olimpik ya mbio za marathon.

Yifter amekuwa pia kocha wa timu ya mbio za nyika ya Ethiopia ilioshinda medali zote 4 za dhahabu za mkimbiaji binafsi huko Edinburgh,Scotland.

Yifter alishinda medali ya shaba katika michezo iliotangulia ya Munich,1972 na kama wanariadha wengi wa Afrika,Miruz Yifter, alikosa kushiriki katika michezo ya olimpik ya Montreal, 1976 kutokana na mgomo wa nchi za kiafrika pamoja na ethiopia dhidi ya michezo ile.ilikua kulalamika kuruhusiwa NZ kushiriki licha ya kutuma timu yake ya rugby nchini Afrika kusini, muda mfupi baada ya machafuko ya Soweto, 1976.

Nguvu za riadha za ethiopia zilizorota mnamo miaka ya 1980 kufuatia kugomea michezo ya Los Angeles, 1984 na ile ya seoul, 1988.

Bendera ya Ethiopia mjini beijing itapepewa na Gebreselassie akishirikiana na kenenisa Bekele na wasichana wake wakali akina Turenesh Dibaba.

Na kwa taarifa hiyo ya kutia moyo kutoka kwa wanariadha wa kenya na Ethiopia, ndio sina budi bali kuishia hapo kwa leo.