Michezo wiki hii | Michezo | DW | 14.03.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michezo wiki hii

Wachezaji 7 wa timu ya Kuba watorokea Marekani na FIFA yaandaa kombe la mashirikisho Afrika Kusini.

Katika ulimwengu wa michezo wiki hii : Umoja wa ulaya unajaribu kuzuwia idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi za Ulaya,nini hatima ya timu ya taifa ya Kuba baada ya wachezaji wake 7 kutorokea Marekani na vipi FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni linavyojiandaa kwa Kombe la mashirikisho-Confederations Cup mwakani-mwaka kabla firimbi kulia kuanzisha kombe la dunia nchini Afrika kusini na la kwanza barani Afrika.

Afisa wa hadhi ya juu wa Umoja wa Ulaya amearifu kwamba mpango wa FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni kurejesha tena vikomo vya idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoruhusiwa kuchezea klabu za ulaya hauna nafasi ya kushinda .Aliungamkono afisa huyo utaratibu wa UEFA-shirikisho la dimba la ulaya la kuwa na mastadi wa dimba waliofunzwa huku huku Ulaya.

Mwishoni mwa mwaka uliopita, rais wa FIFA Sepp Blatter alisema anataka kuwa na mfumo ambao wachezaji 6 kati ya 11 wa timu wawe wa nyumbani na waliobakia waweza kuwawakigeni.Hukumu maarufu ya bosman juu ya swali hilo imesema ubaguzi chini ya msingi ya uraia katika dimba ni kinyume na sheria.Kuwa na mfunmo ambao wachezaji 6 wawe wa nyumbani na 5 wa ugenini ni ubaguzi ulio dhahiri-shahiri-kamishna wa michezo wa Umoja wa Ulaya Jan Figel alisema.

Kama ilivyo kawaida mwaka kabla kuanza kwa kombe la dunia la FIFA huwa zamu ya kombe la mashirikisho-Confederations Cup ili kufungua pazia mwaka mmoja baadae kwa kombe la dunia.FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni kwahivyo, imetangaza mipango ya aina mbili kwa kombe la mashirikisho litakaloanza nchini afrika kusini Juni 14 hadi 28.Kombe hilo litaigharimu FIFA kitita cha dala milioni 17.6 kuliandaa huku mshindi atapewa dala milioni 3.75.

Timu ya taifa ya Kuba imepatwa kati ya wiki hii na msukosuko mwengine ikiania tiketi yake kwa michezo ijayo yadimba la Olimpik huko Beijing.Kisa ni nini wachezaji 7 wa kikosi chao cha timu ya taifa chini ya umri wa miaka 23 waliamua kutorokea marekani.Wachezaji hao 7 walitoweka hotelini pale timu yao ilipokua huko Florida kushiriki katika kinyanganyiro cha kuania tiketi ya dimba la olimpik kati ya wiki hii.

Kwanza wachezaji 5 waliiacha mkono timu baada

►◄

Mabingwa wa Ujerumani VFB Stuttgart wanafanyiwa marekebisho ya uwanja wao wa Daimler Stadium.Ujenzi mpya wa uwanja huo utaamuluiwa rasmi hapo April 24 na baraza la jiji la Stuttgart.

Msemaji wa jiji la Stuttgart amethibitisha taarifa hiyo hapo jana .Jumla ya Eurto milioni 73,2 zitagharimia matengenezo hayo na Stuttgart yenyewe itachangia euro milioni 27 katika ujenzi huo mpya.Kwavile ile sehemu ya riadha itaondoshwa uwanjani humo,huo utakua pia mwisho wa jiji la stuttgart kuwa kituo cha mashimndano ya riadha ya kila mwaka.Daimler-Stadium iliandaa mashindano ya ubingwa wa riadha 1993 ambamo muethiopia Haile Gebreselassie alianza enzi yake ya kutamba.

Wakati Stuttgart-mabingwa wa Bundesliga leo wamecheza na Bochum na viongozi wa ligi-Bayern munich walikuwa na miadi na Energie Cottbus, macho ya mashabiki yanakodolewa mapambano 2 ya hapo kesho:

Werder breem ilioachwa nyuma hadi pointi 7 katika ngazi ya Ligi kati yake na B.Munich kesho itakuwa nyumbani kuchuana na Wolfsburg wakati Bayer Leverkusen iliokata tiketi yake kati ya wiki hii ya robo-finali ya kombe la ulaya la UEFA inacheza na Nüremberg.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com