1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo mwishoni mwa wiki

23 Januari 2009

Ni zamu ya vikombe vya Taifa huko Uingereza na Ufaransa.Kom,be la afrika la vijana Kigali.

https://p.dw.com/p/GeuE

Bundesliga-Ligi ya Ujerumani ikijiandaa kuanza duru yake ya pili mwishoni mwa wiki ijayo baada ya likizo za X-masi na mwaka mpya, timu mbali mbali zimekuwa zikijiimarisha kwa duru hiyo.Baada ya FC Cologne,kujiimarisha kwa Mghana Boetang na Lukas Podolski,Hamburg inaachana na mchezaji wake wa kiungo Nigel de Jong atakaehamia Manchester City,iliohanikiza karibuni kwa kumvutia stadi wa Brazil,Kaka, kwa hadi dala milioni 150.

Mwishoni mwa wiki hii,mbali na Ligi ya itali-Serie A, ni zamu ya Kombe la FA-shirikisho la dimba.Huko Kigali,Ruanda kinyanganyiro cha Kombe la vijana la Afrika chini ya umri wa miaka 20 kinaendelea huku chipukizi wa Afrika Kusini wakitamba.

Kombe la vijana la Afrika nchini Ruanda linaendelea na Afrika kusini ina matumaini ya kucheza nusu-finali baada ya kuitoa Nigeria kwa mabao 2:1.

Mchezaji wa kiungo wa Hammburg ,Nigel de Jong, anahamia Manchester City kwa kitita cha fedha kisichojulikana-kwa muujibu wa Manchester City, de Jong alieichezea Holland mara 29, amefungishwa mkataba wa miaka 4 na nusu.

de Jong alikosa kucheza sehemu kubwa ya duru ya kwanza ya Bundesliga kwa kuumia goti na ni karibuni hivi amerejea kucheza.Amekuwa akiichezea Hamburg miaka mitatu iliopita.

Katika kinyanganyiro cha mwishoni mwa wiki hii cha Kombe la Uingereza la FA,Manchester United, ina miadi na Tottenham Hotspur.Potsmouth inacheza na Swansea wakati Chelsea iko nyumbani na Ipswich Town.Wolverhampton Wanderers wanapambana na Middlesbrough.

Kesho itakua zamu ya Arsenal kuitembelea Cardif City wakati mahasimu wao katika kinyanganyiro cha Premier League-Liverpool watatimuana kesho na Everton.

Katika Ligi ya Ufaransa,Olympique Lyon inacheza leo na Concarneau katika kundi la timu 32 zilizobakia mashindanoni.Stade rennes inapambana na st.Etienne.

Katika changamoto za ligi ya Itali,Reggina inacheza leo na Chievo wakati Juventus inakutana na Fiorentina.

Kesho Bolognia inataembelewa na AC Milan wakati Inter Milan mahasimu wao wa mtaani wanawapokea Sampdoria.Siena pia iko nyumbani ikicheza na Udinese.Napoli inapambana na AS Roma.

Huko Spain,Villareal wana miadi leo na Osasuna wakati viongozi wa ligi FC Barcelona wanapambana na Numancia.

Kesho jumapili Getafe itachuana na Sporting Gijon wakati malaga ina miadi na Atletico Madrid.

Real Mallorca wanacheza na Valencia.Espanyol inaitembelea Real Valladolid.