Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 12.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Nani kati ya B.Munich na Hoffenheim ataibuka kileleni ?

default

Kinyanganiyro :Munich na Hoffenheim

Baada ya changamoto za kati ya wiki za Champions League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya, timu mashuhuri za Ulaya zinarudi uwanjani kwa mapambano ya mwisho kabla X-masi na kuamua nani mabingwa wa nusu-msimu: Katika Bundesliga-ligi ya Ujerumani leo ni leo -asemae kesho muongo:Nani ataibuka bingwa wa nusu msimu kati ya mabingwa hasa Bayern Munich na chipukizi Hoffenheim ?

Changamoto kali kama hiyo inatazamiwa katika La Liga- ligi ya Spain baina ya mabingwa Real Madrid waliomtimua kati ya wiki kocha wao mjerumani Bernd Schuster na FC Barcelona iliofungua mwanya kileleni hadi pointi 9.Real lazima ishinde leo nyumbani kuweka hayi ubingwa.Ama katika Premier League,FC Liverpool inayoongoza kwa pointi 1 inaisubiri leo hull City wakati mahasimu wao kileleni Chelsea wana miadi kesho jumapili na Westham.

Katika Bundesliga, inaamuliwa jioni hii iwapo ni mabingwa Bayern Munich au chipukizi waliopanda msimu huu tu daraja ya kwanza Hoffenheim,wataibuka leo kileleni mwa ngazi ya Bundesliga na hivyo kutawazwa mabingwa wa duru ya kwanza ya msimu kabla ya likizo ya X-masi na mwaka mpya:

Bayern munich ilitamba kati ya wiki katika champions League na mwishoni mwa wiki iliopita ilitia bao dakika ya mwisho kuipokonya Hoffenheim pointi 3.Hatahivyo, Hoffenheim inaongoza leo orodha ya Ligi kwa magoli na mshindi leo wa magoli zaidi atakwenda likizoni akiwa bingwa wa duru ya kwanza.

Munich imedai inataka kuvaa taji hilo na halkadhalika , Hoffenheim.Hoffenheim, kabla kuingia uwanjani kesho kupambana na Schalke, ilitangaza kati ya wiki imemuajiri kipa wa zamani wa akiba wa timu ya Taifa na wa Stuttgart-Timo Hildebrand.Wanamuajiri kutoka Valencia,Spian.Alijiounga na klabu hiyo ya Spian, hapo 2007.

Mahasimu wa Hoffeheim kesho wakicheza nyumbani, ni schalke wakati Bayern Munich wana miadi na Stuttgart.Matumaini ya kutamba kwa Munich ni makubwa na hasa baada ya kuitandika Olympique Lyon ya Ufaransa kati ya wiki mabao 3-2 kwenye champions League huko Lyon.Nafasi ya 3 inaendelea kunyatia Bayer Leverkusen iliopo pointi 3 tu nyuma ya timu hizo mbili.

Kwenye Premier League- Ligi ya Uingereza, Arsenal inachuana jumamosi hii na Middelesbrough wakati Aston villa inapambana na Bolton Wanderes.Viongozi wa Ligi, Liverpool wanawakaribisha nyumbani Hull City .Manchester United inaonana na Tottenham Hotspurs kabla ya kesho Chelsea, kutimiza miadi yao na West Ham na Portsmouth na New castle United.

zahama itakuwa pia leo mjini Madrid kati ya mabingwa Real waliopepesuka msimu huu hadi kubidi kumtimua kocha wao kati ya wiki wakicheza na viongozi wa Ligi FC Barcelona.Barcelona inaongoza Ligi na baada ya pigo ililopata Real la mabao 4-3 kutoka sevilla, leo lazima ishinde.Chini ya kocha mpya Ramos, Real imekamia kutoivika Barcelona taji na mapema.Real ina hamu ya kuendeleza ushindi wake wa kati ya wiki katika champions League ilipoirarua St.Petersberg ya Russia kwa mabao 3-0.Spian nzima itaukodolea macho mpambano huu.

Katika serie A,mapigo mawili mfululizo iliopata Inter Milan pamoja na kutimuliwa nje ya champions League,hakujamkatisha tamaa kocha wa Inter ,mreno Jose Mourinho.Kesho Inter Milan ina miadi na Chievo inayoburura mkia wa Ligi. Inter Milan inatumai bila ya taabu itatamba.Juventus iliopo nafasi ya pili ya ngazi ya Serie A, inapambana na AC Milan mjini Turin.As Roma inaikaribisha Cagliari.Palermo wana miadi na Siena.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com