Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 29.08.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Dimba larudi uwanjani baada ya kugubikwa na olimpik.

Munich- Thomas Mueller,

Munich- Thomas Mueller,

Baada ya michezo ya 29 ya olimpik yaBeijing kumalizika rasmi mwishoni mwa juma lililopita na michezo ya olimpik ya walemavu ikikaribia kuanza Septemba 6-17 mjini Beijing, dimba limeanza kukodolewa macho tena kila pembe ya dunia.

Ligi za Ulaya zimerudi uwanja ni mfano wa Bundesliga wiki 2 nyuma.Nchini Spian la Liga na nchini Itali Serie A zinaanza msimu mpya hii leo.

►◄

Tukianza na Bundesliga-ligi ya Ujerumani,mabingwa Bayern Munich watakuwa uwa njani kesho jumapili wakiwakaribisha nyumbani Allianz Arena Hertha Berlin.

Munich inayoongozwa na kocha mpya Jurgen klinsmann, inahitaji kesho ushindi na pointi 3 baada ya kumudu sare tu ya bao 1:1 katika mapambano yake 2 yaliopita.Wakiteleza nyumbani kesho au wakitoka sare tena kwa mara ya 3,shoka litanolewa kuanza kumfyeka Klinsmann aliepata umaarufu pale alipoiongoza ujerumani hadi nafasi ya 3 ya kombe la dunia 2006 nyumbani Ujerumani.

Munich wiki hii ilijiimarisha kwa kumuajiri kutoka AC Milan beki mashuhuri wa Itali-Massimo Doddo.Doddo aliichezea Itali katika kombe lililopita la dunia ilipoibuka mabingwa.

Mpambano wapili kesho ni kati ya Stuttgart na Hannover.

Leo Armenia Bielefeld inachuana na Hamburg katika changamoto ya majirani wa kaskazini wenyewe kwa wenyewe.Leverkuesen iko nyumbani ikicheza na chipukizi Hoffenheim wanaoongoza Ligi hii licha ya kwamba wamepanda msimu huu tu daraja ya kwanza.

Werder bremen wanaitembelea leo B.moenchengladbach huku Energie Cottbus ikicheza nyumbani na B.Dortmund.Schalke iliotimuliwa kati ya wiki nje ya champions League Athletico Madrid ilipochapwa mabao 4:1, ina miadi na jirani zao Bochum.Wolfsburg inakamilisha lałenda ya Bundesliga leo kwa miadi na Eintracht Frankfurt.Cologne na ilikua jana uwanjani na Karlsruhe.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza, Arsenal inaonana leo na New Castle United.Wakati Bolton Wonderes wana changamoto na West Albion

Wigan Athletic inakaribishwa na Hull City.Everton ina miadi na Portsmouth.Everton iliridhia wiki hii kumfungisha mkataba louis Saha kwa kitita kisichojulikana.Saha akiichezea Manchester united na akiwa na umri wa miaka 30 anafunga mkataba wa miaka 2. Saha amefunga mabao 42 alipoichezea MANU mara 124.

Kesho jumapili Chelsea inapambana na Tottenham Hotspur wakati Manchester city inaizuru Sunderland kabla ya liverpool kuzima vishindo vya Aston villa.

Katika La Liga-ligi ya spian,leo kuna changamoto 2 huku kalenda ndefu ikiahirishwa hadi kesho:

Espanyol ina miadi na Real Valladolid wakati Valencia wanapapurana na Real Mallorca. Real madrid itakua uwanjani kesho ikikutana na mahasimu wake wakubwa Deportivo la Coruna.

Serie A ni ligi ya mabingwa wa dunia-Itali.Leo pia inaanza kwa mapambano 2-Udinese ikicheza na Perlamo huku Sampdoria ikiikaribisha nyumbani Inter Milan.

Mabingwa AC milan wanaanza kesho kutetea taji lao baada ya kumuajiri kutoka Barcelona,Ronaldinho.Mahasimu wao ni Bologna.As Roma wanaonana na Napoli.Kesho Juventus inaitembelea Fiorentina.