Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 11.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Mwenge wa olimpik wawasili jumapili Dar-es-salaam na London na mbio za marathon .

Mwenge wa olimpik kwa michezo ya Beijing unawasili Dar-es-salaam,Tanzania hapo kesho na katibu mkuu wa Kamati ya Olimpik ya Taifa, Philbert Bayi aiambia Deutche Welle "maandalio yamekamilika na kwanini mji wa Dar-es-salaam,umechaguliwa.

Kesho pia ni mbio za London marathon zikishirikisha mbali ya wanariadha wa Kenya na Ethiopia, bali pia kikosi maalmu cha wamasai 6 kutoka Tanzania .

►◄

Baada ya visa vilivyouandama mwenge wa Olimpik wa michezo ya mwaka huu ya Beijing huko Ugiriki,London,Paris, San Francisco na jana mjini Buenos Aires,mwenge wa olimpik unawasili kesho Tanzania.

Tanzania imejiandaa tangu Januari mwaka huu kuupokea mwenge huo. Sasa asema Katibu Mkuu wa Kamati ya olimpik ya Tanzania,bingwa wa zamani wa rekodi ya dunia mita 1.500 Philbert Bayi kilichobaki ni kuanzisha tu mbio hizo za Olimpik mjini Dar-es-salaam.Kwanza anaelezea hivi jinsi maandalio yalivyopangwa na halafu kwanini Afrika nzima ni jiji la Dar-es-salaam pekee limepewa heshima hiyo:

Ulimwengu mzima unakodoa macho kuona iwapo visa vilivyopita miji mingine vya kuzifuja mbio za mwenge wa olimpik vitaonekana kesho hata Dar-es-salaam.

Miji mengine ya Afrika iliowahi kutembeza mwenge wa olimpik ni Cairo,Misri na Pretoria,Afrika kusini.

Kesho ni mbio za london marathon na miongoni mwa waliojinoa kwa mbio hizo za maili 26 ni wamasai 6 kutoka Masaimara,Tanzania.Wao hawagombei kitita cha fedha cha mshindi wa kwanza ingawa hawatakikataa wakipewa,la hasha, hawataki hata rekodi ya mbio hizo, bali azma yao ni kukimbia na kukusanya fedha kwa mradi wa maji kijijini mwao.Mbio zao zitamalizika pale mfereji ukianza kuchuchirika maji kijijini mwao.

Kwa wanariadha kama bingwa mtetezi wa mbio hizi Martin Lel kutoka Kenya, hawataki kasoro ya ushindi na kitita kikubwa cha mshindi wa kwanza, wapili na watatu.Martin Lel ni bingwa mwaka 2005 na alishinda tena mwaka jana 2007.Anadai "mramba asali-harambi mara moja."

Lel na wakenya wenzake kiasi 12 hivi walifanya mazowezi yao huko namibia kabla kuwasili London kwa changamoto ya kesho.Nyumbani Kenya ilikua vigumu kufanya mazowezi kufuatia machafuko ya uchaguzi ya hapo desemba mwaka jana.

Upabde wa wasichana matumaini ya ushindi anayo Muethiopia Geta Wami na hasa kwa kuwa mwenyeji bingwa wa rekodi ya dunia Paula redcliffe hatakimbia.

Katika medani ya dimba ,Bundesliga na hata Premier League zimerudi uwanjani baada ya changamoto za champions League na kombe la ulaya la UEFA kati ya wiki:

Bayern munich ilioitoa Getafe ya Spian na kukata tiketi yake ya nusu-finali ya kombe la UEFA inarudi kesho uwanjani ikiwa na miadi na Borussia Dortmund.Bayer Leverkusen ina miadi na mabingwa Stuttgart.Bremen inaingia leo uwanjani kuchuana na Schalke wakati hamburg inaumana na Duisburg.Katika premier League, huko Uingereza, macho yanakodolewa mpambano wa kesho jumapili kati ya Manchester united na Arsenal.Chelsea itakuwa uwanjani jumatatu ikichuana na Wigan Athletic.

Liverpool ina miadi kesho na Blackburn Rovers.