Michezo mwishoni mwa wiki | Michezo | DW | 17.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Michezo mwishoni mwa wiki

Katika Bundesliga, Bayern munich inaitembelea Bremen wakati katika Premier-League Manchester United,mabingwa wana miadi na Manchester City.

Katika changamoto za Bundesliga, jumamosi hii timu nyengine 2 zinazopigiwa upatu kuibuka mabingwa-Bayern Munich na Werder Bremen zinapambana mjini Bremen.Miroslav Klose,mshambulizi wa timu ya Taifa aliejiunga na Munich msimu huu kutoka Bremen, atakua na kazi ngumu mbele ya mashabiki wa Bremen aliowaacha mkono.

Katika premier League-ligi ya Uingereza, Liverpool ina miadi na Chelsea wakati mabingwa Manchester, wanaumana na mahasimu wao wa mtaani Manchester city.

Macho halkadhalika, yatakodolewa mpambano kati ya mabingwa Stuttgar na Hertha Berlin katika uwanja wa Olimpik wa Berlin.Armenia Bielefeld inatazamiwa kutamba tena nyumbani ikikaribisha E.Frankfurt wakati Hansa Rostock iliokomewa mabao 3-0 na bayern munich jumamosi iliopita haimudu pigo jengine na mara hii nyumbani kutoka Nüremberg.Duisburg inaumana na Wolfsburg.

Kesho duru ya mwishoni mwa wiki hii itakamilishwa kwa m apambano 2: Hamburg wataikaribisha nyumbani Bayer Leverkusen wakati Energie Cottbus itakamilisha dibaji kwa mpambano na Bochum.

Ama katika Ligi ya Uingereza,ndugu 2 wa mtaani wanaumana leo-Manchester United-mabingwa wanahitaji pointi 3 kutoka Manchester City,lakini wanateremka uwanjani bila majogoo wao Wayne Rooney alieumia na Christian ronaldo aliefungiwa kucheza.Viongozi wa Ligi Everton watumai kubakia kileleni wakiitimua Reading iliomudu suluhu na Manchester mwishoni mwa wiki iliopita.

Katika kinyan’ganyiro cha kuania kombe la klabu bingwa barani Afrika,Al Hilal ya Sudan, inaikaribisha leo mabingwa Al Ahly ya Misri mjiniOmduraman, mbele ya mashabiki 35.000 ili kukata tiketi ya nusu-finali.Al hilal ikiimarishwa na mastadi wa Nigeria na Msumbiji wanaamin I waweza kuzuwia pointi 3 zisiondoke Khartoum ,kuelekea Cairo.

Kesho, ASEC Abidjan ya Corte d’Iviore, inawakirimu wageni wao Esperence ya Tunisia.Viongozi wa kundi A,Etoile du Sahel ya Tunisia, wameshakata tiketi ya nusu-finali na hakuna shaka watachukua pointi 3 nyumbani leo kutoka kikapu cha FAR Rabat ya Morocco.

Ni vigumu kuagua changamoto kati ya JS Kabylie ya Algeria na Al Ittihad ya libya iliopo nafasi ya pili.

Stadi mpya wa Werder Bremen,Boubacar Sanogo ameitwa kujiunga na kikosi cha Ivory Coast kwa changamoto ya kirafiki ya wiki ijayo na Misri mjini Paris.Sanogo anajaza pengo lililoachwa na Aruna Dindane alieumia.Tangu Misri hata Ivory Coast zinatumia changamoto hii kujiandaa kwa tikiti za kombe lijalo la Afrika la mataifa nchini Ghana.

Ujerumani itateremka nayo bila ya nahodha wake Michael Ballack na mshambulizi wa klabu bingwa-Stuttgart –Mario Gomez watakapoumana na Uingereza uwanjani Wembley jumatano ijayo.Ballack bado hajapona wakati Gomez-mchezaji wa mwaka wa Ujerumani,ameumia .

 • Tarehe 17.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbH
 • Tarehe 17.08.2007
 • Mwandishi Ramadhan Ali
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHbH