1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michezo mwishoni mwa Juma

Mohammed AbdulRahman13 Novemba 2006

Msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga wabadilika na uongozi sasa umo mikononi mwa Stuttgart. Al Ahly ya Misri ni mabingwa tena wa Afrika.

https://p.dw.com/p/CHcx
Mambo yalivyokua katika pambano kati ya Hannover (wenye fulana nyekundu) na Stuttgart. Matokeo ya 2-1 yaliipa nafasi Stuttgart kutwaa uongozi wa ligi hiyo.
Mambo yalivyokua katika pambano kati ya Hannover (wenye fulana nyekundu) na Stuttgart. Matokeo ya 2-1 yaliipa nafasi Stuttgart kutwaa uongozi wa ligi hiyo.Picha: AP

Ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga iliingia katika usiku yake ya 12, pakizidi kushuhudiwa shauku na msisimko baada ya matokeo ya mwishoni mwa Juma. Werder Bremen sasa imepoteza uongozi , Kwani baada ya kufungwa katikauwanja wa nyumbani mabao 3-1 na Dortmund,Stuttgart iliokua ikiiandama imechukua usukani kufuatia ushindi wa bao na kuitangulia Bremen kwa pointi moja. Stuttgart ina pointi 24 . Bremen ikiwa nafasi ya pili inaitangulia Schalke kwa magoli –zote zikiwa na pointi 23 kila moja. Schalke iliibwagha Mainz mabao 4-0 . Kevin Kuranyi aliyekosolewa mno katika mechi zilizopita, na hata kususia kuzungumza na vyombo vya habari , aliwasuta wakosoaji wake alipofunga mabao mawili katika ushindi huo, huku mawili mengine yakipachikwa na halil Alkintop.

Mabingwa watetezi ambao hadi wiki iliopita, walikua wako tafauti ya pointi 6 na Bremen walipunguza mwanya hadi pointi tatu walipoifunga Bayer Leverkusen nyumbani mabao 3-2 katika mechi ya kukata na shoka. .ArmeniaBielefeld chini ya Kocha Thomas von Hessen iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Eintracht Frankfurt .

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ujerumani Jens Lehmann atalikosa pambano la Jumatano la kuwania nafasi ya kushiriki fainali za kombe la Ulaya 2008, dhidi ya Cyprus mjini Nikosia kwa sababu ya mafua. Wakati huo huo kukiwa na hofu pia ya kushiriki kwa wachezaji wa kiungo Bernd Schneider na Piotr Trochowski kwa sababu ya majeraha. Kuungua mafua kwa Lehmann kulimkosesha pia pambano la jana kati ya timu yake ya Arsenal na Liverpool katika ligi kuu ya England ambapo Arsenal maarufu kwa jina jengine la Gunners waliibuka na ushindi wa mabao 3-0. Huenda langoni katika mechi dhidi ya Cyprus akaweko mlinda mlango wa Stuttgart Timo Hildebrand.

Katika Ligi kuu ya England -Premier League, Manchester United inaendelea kujiimarisha zaidi katika uongozi wa ligi hiyo. Mwishoni mwa Juma iliandika pointi tatu nyengine baada ya kuibwaga Blackburn kwa bao pekeelililopachikwa na Louis Saha katika dakika ya64. Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha wa Manchester United Sir Alex Furguson alisema vijanawake wamethibitishwa kwamba wanaweza kuutwaa ubingwamsimu huu, hasa kwa kiuwa wameiandama Chelsea-mabingwawatetezi tangu mwanzoni. Chelsea kwa upande wakeiliipa funzo Watford la mabao 4 kwa sifuri. Katika mechi nyengine za ligi hiyo Everton ilijikutaikifungwa na Aston Villa 1-0 , Portsmouthikalazimishwa sare nyumbani na Fulham 1-1, MachesterCity ilimaliza sare bila kufungana na New Castle na Middlesbrough ikaibwaga West Ham United bao 1-0.

Barani Afrika Al Ahly ya Misri imesawazisha rekodi yawapinzani wao Zamalek na kuutwaa ubingwa wa Afrika–Champions League-kwa mara ya tano, baada ya ushindiwa bao 1-0 mbele ya Sfaxien ya Tunisia kwao mjinitunis. Itakumbukwa mchezo wa kwanza huko Kairo majuma mawili yaliopita ulimalizika sare ya bao moja kwa moja na kuwapa matumaini Sfaxien kwamba wangewezakuzusha maajabu nyumbani, lakini haikua hivyo, kwani bao lililofungwa na Mohamed Aboutrika baada yakumalizia pasi safi ya mchezaji wa kimataifa wa Angola Flavio lilitosha kuwanyamazisha watazamaji 52,000waliofurika uwanjani na kuwanyima Sfaxien nafasi yakushinda kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Mbali na kitita cha dola milioni moja, Al Ahly iliokuaikitetea ubingwa huo na inayo sherehekea miaka 100tangu kuundwa , itaiwakilisha afrika katika mashindanoya kilabu bingwa za mabara, yatakayofanyika Japan mwezi ujao. Ni ushindi wa tatu kwa kocha Manuel Jose akiwa na Al Ahly baada ya 2001 na kulinyakuapia kombe hilo mwaka jana. Ni kilabu ya tatu, katikakipindi cha zaidi ya miaka 40 kuutetea ubingwa huo waAfrika kwa ufanisi na hivyo kuunyakua mara mbilimfululizo .

Rais wa Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF, IssaHayatou ametangaza kwamba atagombea tena nafasi hiyopale kipindi chake cha tatu kitakapomalizika 2009.Hayatou amesema anataka kuwa katika wadhifa huokuyakaribisha mashindano ya kwanza ya fainali yakombe la kandanda la dunia 2010 yatakayofanyika kwamara ya kwanza kabisa barani afrika nchini Afrikakusini. Hayatou kutoka Kamerun na mwenye umri wamiaka 59, alichaguliwa mara ya kwanza kuwa Rais wa CAf 1988 baada ya kifo cha Ydnekatchew Tessema kutokaEthiopia. Miongoni mwa mafanikio ya Hayatou nikupigania nafasi zaidi kwa Afrika katika fainali zakombe la dunia, kutoka mbili 1990 hadi tano 1998.

Katika ringi ya ubondia,Wladimir Klitschko wa Ukraine amefanikiwa kuliteteataji lake la ubingwa wa uzito wa juu duniani katikaShirikisho la ndondi la kimataifa –IBF. Katika pambanolake la kwanza la kuutetea ubingwa huo Klitschko alimtwanga mpinzani wake Calvin Brock wa Marekanikatika raundi ya saba. Klitschko ameshinda mapambano 47 aliyopigana hadi sasa kishindwa mara tatu, wakati kushindwa kwa Brock jana ni kwa kwanza katikamapambano yake 30. Miongoni mwa watazamaji 14,260 waliofurika katika ukumbi wa Madison Square Gardenmjini Newyork kujionea pambano hilo, ni pamoja nabingwa wa zamani wa dunia na Mfalme wa masumbwi,Muhammad Ali.

Tennis: Roger Federer wa Uswisi alianza kwamatumaini mashindanmo ya Tennis ya Shanghai hukoChina alipofanikiwa kumtoa bingwa mtetezi wamashindano hayo David Nalbadian wa Argentina , aliyemtoa Federer katika fainali ya 2005. Alikua ni Nalbandian aliyeanza kwa kishindo alipoongoza katika seti ya kwanza kwa 6-3 , kabla ya mambo kumuendea kombo na Federer kushinda seti mbili zilizosalia kwa matokeo ya 6-1 na tena 6-1, mchezo uliochukua muda wa saa 1 na dakika 27. Katika mechi nyengine Mmarekani Andy Roddick akamsinda Ivan Ljubick kutoka Kroatia seti mbili kwa moja, kwa matokeo ya 6-4, 6-7 na 6-1. Kundi linalojulikana kama kundi la dhahabu akiwemo anayeshika nafasi ya pili duniani Rafael Nadal wa Uhispania inaanza leo.