1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 31 ya mapinduzi ya kiislam nchini Iran

Oumilkher Hamidou11 Februari 2010

Rais Ahmadinedjad anassema nchi yake ina uwezo wa kurtubisha hadi asili mia 80 ya maadini ya Uranium

https://p.dw.com/p/Lyd9

Malaki ya wairan wamekusanyika hii leo mjini Teheran na kote nchini humo kuadhimisha miaka 31 ya mapinduzi ya kiislam,pakiwepo ulinzi mkali wa vikosi vya usalama vilivyopania kuzuwia maandamano ya upande wa upinzani.

Umati mkubwa wa watu wamekusanyika tangu asubuhi katika uwanja wa uhuru-Azadi na katika maeneo mengine ya mji mkuu Teheran,wakipeperusha vibendera vyenye rangi ya kijani,nyeupe na nyekundu.

Waaandamanaji walikua wakipaza sauti kushadidia unyenyekevu wao kwa kiongozi wa mapinduzi ya kiislam Ali Khamanei.

Akihutubia umati huo wa watu,rais Mahmoud Ahmadinedjad amesema Iran inapanga kuzidisha mara tatu hivi karibuni kiwango cha uranium inayorutubishwa katika eneo, la kati la Natanz na kufikia hadi asili mia 3.5.

"Iran imerutubisha na kujaza asili mia 20 ya maadini ya Uranium na ina uwezo wa kurutubisha hata asili mia 80,lakini hatutofanya hivyo kwasababu hatuihitaji"-amesema rais Ahmedinedjad.

Rais Mahmoud Ahmedinedjad anasema:

"Kwa msaada wa Mwenye enzi Mungu na kwa baraza za mamilioni ya wananchi wa iran,Bahram 22 hii ni mwanzo wa mapainduzi ya kiislam ulimwenghuni na mwanzo wa kuwepo haki katika dunia."

Rais Mahmoud Ahmedinedjad amemkosoa rais Barack Obama wa Marekani na kusema tunanukuu: matumaini mema aliyoyazusha,yanaelekea kufifia."Mwisho wa kumnukuu.

Iran Rede von Ahmadinedschad
Rais Ahmadinedjad wa IranPicha: AP

Sherehe za miaka 31 ya mapinduzi ya kiislam zinafanyika huku kukiwa na ulinzi mkali. Vikosi vya usalama vinapiga doria katika uwanja wa uhuru- Azadi na katika kila pembe ya mji mkuu.

Viongozi wa upinzani,Mohammed Khatami na Mehdi Karoubi wameshambuliwa japo kama hawajajeruhiwa na waliovalia kiraia.Walikua ndani ya magari yao wakielekea katika maandamano kuadhimisha miaka 31 ya mapinduzi ya kiislam.

Wakati huo huo kamata kamata imeshika kasi mjini Teheran: mjukuu wa Ayatollah Ruhollah Khomeini na mumewe -Zahra Eshraqi na Mohammed Reza Khatami ambae ni ndugu wa rais mpenda mageuzi wa zamani Mohammad Khatami wamekamatwa.Hata mtoto wa kiume wa kiongozi wa upande wa upinzani Mehdi Karoubi amekamatwa.

Hali inatisha na katika wakati ambapo Iran inakabiliwa na vitisho vya kuwekewa vikwazo ziada vya kimataifa kutokana na kukataa kwake kusitisha utaratibu wa kurutubisha maadini ya uranium,serikali ya mjini Teheran imeshaonya haitovumilia hata kidogo kusikia sauti za upande wa upinzani hii leo.

Generali Hossein Hamedani,ambae ni mkuu wa vikosi vya jeshi linaloeneza nadharia ya utawala wa kiislam nchini Iran,ameshasema "hawatovumilia maandamano yoyote ya vuguvugu la kijani."

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Afp,Reuters

Imepitiwa na Abdul-Rahman