Miaka 30 tangu Ukuta wa Berlin ulipoanguka | Makala | DW | 04.11.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Makala

Miaka 30 tangu Ukuta wa Berlin ulipoanguka

Miaka 30 tangu ukuta wa Berlin ulipoanguka, hali ikoje na jinsi hali inavyotokota katika chama cha Christian Democratic Union CDU ni miongoni ma mada zilizogonga vichwa vya habari magazetini.

Tunaanza kwa kumulika miaka 30 tangu ulipoanguka ukuta wa chuma uliokuwa ukiigawa Ulaya kambi mbili, mashariki na magharibi. Gazeti la "Mittelbayerische Zeitung" linaandika. "Miaka 30 tangu ukuta ulipoanguka, furaha na shangwe zilizokuwa zimehanikiza Poland, Hungary, Jamhuri ya Cheki na Slovakia zime zimetoweka. Na huko pia kero na machungu ndio yaliyobakia. Na waziri wakuu wa Hungary Viktor Uruban na Jaroslaw Kaczynski, kiongozi , wenye ushawishi mkubwa nchini Poland hawachoki kuzungumzia kuhusu wasomi wanyonyaji na wananchi waliopokonywa ushindi  mwaka 1989. Ni kiroja kikubwa hiki kwasababu kila wakati ambapo wakaazi wa Poland, Hungary na jamhuri ya Cheki wanajivunia hali nzuri ya kiuchumi ndipo kero na hali ya kuvunjika moyo inapozidi kuwa kubwa dhidi ya kile wanachokiita " mageuzi ya pupa kuelekea magharibi", baada ya mwaka 1989l."

Nani agobee waadhifa wa kansela kutoka vyama vya CDU/CSU

Kinyang'anyiro cha nani anastahiki kuwania kiti cha kansela uchaguzi mkuu utakapoitishwa mwaka 2021 kimeanza ndani ya vyama ndugu vya kihafidhina vya Christian Democratic Union, CDU, na Christian Social Union-CSU. Kansela Angela Merkel ameshasema hatogombea tena wadhifa huo. Hadi wakati huu, mwenyekiti wa chama ndie anaekuwa na jukumu la kugombea wadhifa wa kansela. Lakini hivi sasa sauti zinasikika kupinga utaratibu huo. Gazeti la "Badische Zeitung" linamulika mvutano ndani ya vyama ndugu vya CDU/CSU na kuandika: "Kuna tokota ndani ya vyama ndugu vya  kihafidhina vya CDU-CSU, tena kweli kweli kwasababu lile jopo la kumteuwa mgombea kiti cha kansela ambalo kawaida husifiwa kuwa ni tulivu na lenye nidhamu , halina uongozi imara: Kramp-Karrenbauer hawavutii wapiga kura, Merz anamkosoa Merkel nae Söder anamkaripia Merz awajibike.

Merz lakini ameshasema hataonyamaza mkutano mkuu wa chama utakapoitishwa hivi karibuni-kwa namna hiyo suala la nani atagombea wadhifa wa kansela kwa tikiti ya vyama ndugu vya akihafhidhina bado halikupata jibu. Zahma hii inajiri kataika wakati ambapo muungano unaongoza serikali kuu mjini Berlin unakabiliowa na hatari ya kuvunjika kwasababu ya mvutano kuhusu malipo ya uzeeni-matokeo yake yatakuwa kuitishwa uchaguzi mkuu wa kabla ya wakati."

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Yusuf Saumu