1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miaka 20 baada ya Mauwaji ya halaiki Rwanda

7 Aprili 2014

Katika wakati ambapo Rwanda inatafakari miaka 20 baada ya mauwaji ya halaiki, taasisi ya wanasheria ya Ufaransa imefanikiwa kumhukumu mmojawapo wa waandalizi wa mauaji hayo ya halaiki Pascal Simbikangwa.

https://p.dw.com/p/1Bd19
Majeneza ya wahanga wa mauwajiPicha: Getty Images

Kesi ya kwanza ya mnyarwanda aliyekuwa akituhumiwa kuhisika na mauwaji ya halaiki ni hatua muhimu kwa jopo hilo maalum la mjini Paris linaloshughulikia masuala ya aina hiyo na ambalo linaanza kupanua shughuli zake-anasema naibu mwendesha mashtaka mkuu Aurélia Devos.

Pascal Simbikangwa,myarwanda wa kwanza kuhukumiwa nchini Ufaransa kwa makosa ya kushiriki katika mauwaji ya halaiki ya watu wa kabila la tutsi mnamo mwaka 1994,alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela Marchi 15 iliyopita,na kuipatia jaza ya kwanza taasisi hiyo inayoshughulikia masuala ya mauwaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinaadamumbele ya mahakama ya mjini Paris.

Ikiundwa mapema mwaka 2012,taasisi hiyo imejiwekea lengo la kupambana dhidi ya mitindo ya kutoandamwa kisheria wahalifu wa vita ambao wamekimbilia nchini Ufaransa nchi yenye idadi kubwa ya wahamiaji.

"Ni hatua muhimu" amesema Aurélia Devos ambae ni mkuu wa taasisi hiyo ya masuala ya sheria."Kesi dhidi ya Pascal Simbikangwa imebainisha kwa mkumbo mmoja kwamba ni halali na ni jambo linalowezekana kumfikisha mahakamani nchini Ufaransa mgeni yoyote,kwa makosa aliyoyafanya katika pembe nyengine ya dunia."

Hata hivyo kesi hiyo ya kwanza sio anzilishi,anahisi mwanasheria huyo na kusisitiza kwamba taasisi yake-mojawapo ya mashirika madhubuti barani Ulaya,yenye majaji watatu,wanasheria wawili na wasaidizi wao na wachunguzi 12 wanaokutana tangu mwezi wa februari katika ofisi yao kuu,wanashughulikia masuala tofauti yanayopindukia yale yanayohusiana na Rwanda.

Shabaha ni kurejesha uhusiano pamoja na Ufaransa

Kesi nyingi-27 kati ya 35 wanazozishughulikia zinawahusu watuhumiwa wa mauwaji ya halaiki ya Rwanda waliohamia Ufaransa."Lakini nijuavyo mie haijawahi kuwa taasisi inaoshughulikia suala la Rwanda tu" amehakikisha Aurélia Devos.Mashirika kadhaa yamekuwa yakiituhumu taasisi hiyo tangu ilipoanzishwa kuwa chombo kinachoshughulkia kutuliza uhusiano kati ya Paris na Kigali.

Pascal Simbikangwa
Pascal Simbikangwa ahukumiwa kifungo cha miaka 25 jela nchini UfaransaPicha: picture-alliance/AP Photo

Uhusiano mbaya kati ya Ufaransa na Rwanda ulikwenda umbali wa kuvunjwa uhusiano wa kibalozi kati ya nchi hizo mbili mwezi Novemba mwaka 2006.Uamuzi huo ulipitishwa baada ya jaji mmoja wa kifaransa kutangaza waranti wa kukamatwa maafisa tisa wa Rwanda kuhusiana na uchunguzi wa shambulio la April, sita mwaka 1994 lililopelekea kuuwawa rais wa zamani wa kihutu Juvénal Habyarimana-chanzo cha kuzuka siku ya pili yake mauaji ya halaiki nchini Rwanda.

Watuhumiwa wengine pia wanaandamwa

Katika wakati ambapo Pascal Simbikangwa amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela,mnyarwanda mwengine Charkes Twagira ametiwa korokoroni baada ya kukutikana na hatia ya kuhusika na mauwaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinaadam.

Ruanda-Prozess in Frankfurt
Mafuu ya wahanga wa mauwaji ya halaiki ya RwandaPicha: picture-alliance/dpa

Wanasheria wake wanatumia wakati mwingi kutathmini hali ya isiasa,kihistoria,kiuchumi na kisaikolojia ya nchi ambako uhalifu umetokea.Na kwa upande wa Rwanda mtu anaweza kusema ni kadhia moja inayowahusu watuhumiwa 27.Anasema.Kadhia nyenginezo ambazo wanasheria wa taasisi hiyo wanazishughulikia ni pamoja na ile ya Iraq, Libya,Tchad,Congo Brazaville,jamhuri ya Afrika kati,Cambodjia na Maroko.Na kadha nyengine kadhaa zinazohitaji uchunguzi wa awali.Mojawapo ya kadhia hizo inahusu biashara ya zana za ukaguzi iliyofanywa na kampuni ya Ufaransa Amesys kwa utawala wa zamani wa Muammar Gaddafi nchini Libya-kampuni inayotuhumiwa na mashirika yasiyomilikiwa na serikali,kusaidia katika kuwatesa wapinzani wa serikali.

"Hatujaribu kupanua uwanja wa shughuli zetu-zipo tayari,anasisitiza mwanasheria huyo Aurélia Davos.

Uwaja huo umepata nguvu kutokana na kuongezeka vusa vya uhalifu dhidi ya ubinaadam.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman