Miaka 10 tangu shambulio la 9/11 | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 11.09.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Miaka 10 tangu shambulio la 9/11

Leo ni kumbukumbu ya miaka 10 tangu kutokea shambulio la kigaidi nchini Marekani Septemba 11 mnamo mwaka 2001

default

Eneo la kumbu kumbu, Ground zero mjini New York

Raia nchini humo wanajitayarisha kwa maadhimisho ya siku hii.Katika hotuba yake ya kila wiki, Rais Barack Obama hapo jana alisema kuwa muongo mmoja baadaye Marekani imekuwa na nguvu zaidi, huku kundi la kigaidi la Al Qaeda linaelekea kushindwa

Barack Obama Pressekonferenz Budgetverhandlungen USA Juli 2011

Rais Barack Obama wa Marekani

.

Aligusia hususan kuuliwa kwa kiongozi mkuu wa kundi hilo, Osama bin laden mapema mwaka huu. Rais wa zamani nchini humo, George.W. Bush, aliyekuwa uongozini wakati wa shambulio hilo, alihudhuria sherehe za kuweka shada la maua katika wizara ya ulinzi, Pentagon.

USA Geschichte 11 September 2001 Präsident George Bush erhält Nachricht vor Schulklasse

Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush

Bush alieleza masikitiko yake kwa familia na marafiki za wahanga takriban 3000.

Maadhimisho kadhaa yamepangwa kote nchini hii leo katika kumbukumbu ya siku hii. Wakati huo huo, matayarisho ya kumbukumbu hiyo yamegubikwa na kitisho cha onyo kwa umma kilichotolewa na maafisa wa usalama nchini humo, kinachoaminika kutokana na uwezekano wa mpango wa mashambulio dhidi ya mji wa New York na ama Washington D.C.

Mwandishi: Maryam Abdalla/rtre, ape, afpe, tv
Mhariri: Kitojo Sekione

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com