Mgomo wa wafanyikazi wa Lufthasa kuathiri viwanja vya Frankfurt na Hamburg | Habari za Ulimwengu | DW | 27.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mgomo wa wafanyikazi wa Lufthasa kuathiri viwanja vya Frankfurt na Hamburg

-

BERLIN

Msemaji wa chama cha wafanyikazi nchini Ujerumani VERDI amesema kwamba mgomo unaoanza hapo kesho wa wafanyikazi wa shirika la ndege la Lufthansa utaathiri shughuli za viwanja vya ndege vya Frankfurt na Hamburg.

Msemaji wa chama cha Verdi Harald Reutter amefahamisha kwamba viwanja vingine vya ndege nchini Ujerumani vinavyotoa huduma za shirika hilo kubwa la ndege la Ujerumani pia vitaathirika.

Wafanyikazi elfu 52 wa kampuni ya lufhansa wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 9.8 lakini shirika hilo lilipendekeza mapema mwaka huu kuwaongezea asilimia 6.7.

Wanasiasa nchini Ujerumani wamezitolea mwito pande zote mbili kampuni na wafanyikazi kukaa chini na kufikia maelewano na kumaliza mvutano haraka.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com