1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa treni waepushwa Ujerumani

10 Machi 2008

Mgomo wa taifa zima wa madereva wa treni nchini Ujerumani umeepushwa masaa machache kabla ya kuanza.

https://p.dw.com/p/DLXh

BERLIN

Manfred Schell mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi madereva wa treni nchini Ujerumani GDL ametowa tangazo hilo kufuatia masaa kadhaa ya mazungumzo mjini Berlin.

Hata hivyo shirika la reli laaifa nchini Ujerumani Deutsche Bahn limesema abiria bado wanaweza kukabiliwa na usumbufu wa kuchelewa mno kwa safari za reli kwa sababu makubaliano yao yamechelewa mno kufikiwa kuweza kubadili ratiba ya safari ya dharura na kurudia ile ya kawaida.

Deutsche Bahnn imesema makubaliano tafauti yaliokuwa yakidaiwa na chama cha wafanyakazi madereva wa treni GDL yamekubaliwa na vyama vyengine viwili vya wafanyakazi vinavyowakilisha wafanyakazi wa reli lakini chini ya masharti yanayohakikisha mpango wa msingi kwa waajiriwa wote.

Hapo mwezi wa Januari migomo ya kuonya ilipelekea kufikiwa kwa makubaliano ya awali ya kuongeza mishahara ya madereva kwa asilimia 11 na kupunguza muda wa masaa ya kazi.

Chama cha GDL kilikuwa kimepanga kusitisha safari za treni za abiria, mizigo na treni za vitongoji kwa muda usiojulikana kuanzia leo hii.