1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgomo wa Lufthansa wasimamishwa.

23 Februari 2010

Marubani wa Lufthansa warejea kazini baada ya kugoma kwa siku moja.

https://p.dw.com/p/M8m1
Abiria wakwama kutokana na mgomo.Picha: AP

Ndege za Shirika la ndege la Ujerumani, Lufthansa zimeanza tena safari zake, baada ya marubani wake 4,000 kusimamisha mgomo wao na kurejea kazini usiku wa kuamkia leo. Shirika hilo la Lufthansa lilikuwa limewasilisha amri mahakamani kusimamisha mgomo huo wa siku nne. Chama cha marubani hao Cockpit kikakubali kurejea kazini baada ya kugoma kwa siku moja pekee yake. Makubaliano hayo yanaitisha kuanzishwa kwa majadiliano mara moja na kuzuia kutofanyika kwa mgomo mwingine kabla ya tarehe nane mwezi Machi. Marubani hao wa Lufthansa wanalalamikia kuongezwa mishahara yao kwa asili mia sita pamoja na uhakika wa ajira zao kwa takriban mwaka mmoja. Hata hivyo, mgomo wa wasimamizi wa mawasiliano ya angani nchini Ufaransa uliopangwa kuanza leo, utaendelea. Vile vile uwezekano wa kufanyika kwa mgomo wa wahudumu wa ndege za Shirika la Ndege la Uingereza British Airways, itaendelea kutatiza safari za ndege hapa Ulaya.

Lufthansa / Streik / Pilot
Rubani wa ndege za Lufthansa.Picha: AP