1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgombeaji urais wa mrengo wa kulia Brazil ashambuliwa

7 Septemba 2018

Mgombeaji wa urais wa mrengo wa kulia nchini Brazil Jair Bolsonaro amepigwa risasi na kujeruhiwa alipokuwa kwenye kampeni yake ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/34Sod
Brasilien Messerattacke auf Präsidentschaftskandidaten Jair Bolsonaro
Jair Bolsonaro akiashiria uchungu baada ya kudungwa kisu tumboniPicha: Getty Images/AFP/R. Leite

Kisa hicho ni cha hivi punde kutokea kufuatia kinyang'ang'anyiro hicho , wakati mgombeaji maarufu, aliyekuwa rais na kiongozi wa wafuasi wa mrengo wa kushoto  Luiz Inacio da Silva, akijaribu kutaka kuigombea kutoka gerezani.

Bolsonaro alifanyiwa upasuaji kutokana na majeraha mbalimbali aliyopata na ametajwa kuwa hali yake inaimarika baada ya shambulio hilo lililotokea katika mji wa Juiz de Fora. Picha zilizosambazwa mitandaoni na kwenye televisheni ya kitaifa nchini Brazil zilionesha Bolsonaro akiwa amebebwa mabegani mwa wafuasi wake, kabla ya mwanamume asiyejulikana kumshambulia.

Mwanamume huyo alikamatwa punde tu baada ya kisa hicho. Mshambuliaji huyo ametambuliwa kuwa Adelio Bispo de Oliveira mwenye umri wa miaka arubaini na mwanachama wa chama cha mrengo wa kushoto PSOL tangu mwaka 2004 hadi 2014.

Mkuu wa muungano wa shirikisho la maafisa wa polisi, Luis Boundens amesema baada ya kukamatwa Oliviera alisema kwamba alikuwa akitekeleza agizo kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Polisi wanamfanyia uchunguzi wa akili kubaini iwapo ana akili timamu.

Uchunguzi kufanywa kuhusu kushambuliwa kwa Bolsonaro

Brasilien Präsidentschaftswahlen Kandidat Jair Bolsonaro
Picha: Getty Images/AFP/E. Sa

Bolsonaro ambaye aliwahi kuwa mwanajeshi na mbunge, amekuwa akikosolewa kwa kutoa matamshi ambayo yanasemekana kuwa ni ya kibaguzii. Awali mwanawe Flavio Bolsonaro, alisema kupitia mtandao wake wa Twitter kwamba majeraha ya babake ni mabaya sana tofauti na walivyofikiria.

Msemaji wa Rais ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Rais Michel Temer amekashifu shambulio hilo na kumuagiza Waziri wa Usalama Raul Jungmann kuimarisha usalama kwa wagombeaji, vile vile kuendesha uchunguzi wa kina kuhusiana na kisa hicho.

Wakati huo huo, Mahakama ya juu  ilisema  alhamisi kwamba rais wa zamani  mwanasiasa wa  mrengo wa kushoto   Luiz Inacio da Silva maarufu kwa jina la Lula hafai kuwania kiti hicho cha urais . Lula alipatikana na hatia ya  kupokea rushwa na anatumikia kifungo cha miaka 12 jela.Awamu ya kwanza ya upigaji kura inatarajiwa kufanyika tarehe 7 mwezi ujao.

Mwandishi: Sophia Chinyezi/AFPE

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman