1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mgogoro wa Ukraine waendelea

6 Aprili 2007

Mgogoro wa Ukraine imeingia katika hatua nyingine kutokana na waziri mkuu wa nchi hiyo bwana Viktor Yanukovych kuiomba Austria isuluhishe.

https://p.dw.com/p/CHGn
Viongozi wa Ukraine waziri Mkuu Yanukovych na rais Yushchenko
Viongozi wa Ukraine waziri Mkuu Yanukovych na rais YushchenkoPicha: AP


Bwana Viktor Yanukovych amesema kuwa hatua iliyochukuliwa na rais wa Ukraine bwana Yushenko ya kuvunja bunge na kuitisha uchaguzi mapema si halali.

Akizungumza na wandishi habari bwana Yanukovych alisema kuwa rais Yushenko amekiuka katiba kwa kuitisha uchaguzi mapema.

Waziri mkuu Yanukovych amesema ili kuepusha mgogoro kuendelea kushtadi ameiomba Austria iiingilie kati ili kusuluhisha.

Na ABDU MTULLYA