1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mfumo wa elimu nchini Tanzania

22 Aprili 2013

Nchini Tanzania, Tume ya Vyuo Vikuu Nchini(TCU), imepanga kuanza kuwatathmini wanafunzi wa kujiunga na masomo ya vyuo vikuu kwa kutumia uzoefu wao.

https://p.dw.com/p/18KWE
Wanafunzi wa shule ya msingi nchini Tanzania
Wanafunzi wa shule ya msingi nchini tanzaniaPicha: DW/Thomas Kohlmann

Utaratibu huo utakaoanza mwaka huu wa masomo 2013/14, utakuwa ukiwahusisha wale ambao elimu yao imeishia darasa la saba na kuendelea, lakini walikosa sifa ya kuendelea na masomo kwa ngazi ya chuo kikuu.

Kupitia utaratibu huo mpya, mtahiniwa atajiunga na Chuo Kikuu kulingana na fani atakayoiomba na atatakiwa kufanya mitihani mitatu na kufaulu kwa wastani wa daraja la B. Hata hivyo hayo yamezusha mjadala miongoni mwa baadhi ya watu wakihoji kwamba tayari mfumo wa elimu uko katika hali mbaya, hasa kutokana na matokeo ya mwaka huu ya mtihani wa kidato cha nne. Amina Abubakar amezungumza na Mdau wa Elimu anayefanya kazi na shirika la "Haki elimu" nchini Tanzania Nyanda Shuli, ambaye kwanza anaelezea maoni yake juu ya hatua hiyo.Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman