Mfumo Maarufu wa Ulaya wa Marejeleo ya Lugha | Njia rahisi | DW | 14.06.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Njia rahisi

Mfumo Maarufu wa Ulaya wa Marejeleo ya Lugha

Mfumo wa Ulaya unatoa msingi wa umoja wa kujifunza lugha kote Ulaya. Katika viwango sita vilivyosanifishwa, unaelezea stadi alizo nazo mwanafunzi kwenye kila hatua anapoendelea.

Kiwango cha A1 – Kuanza
Jifunze jinsi ya kusema vitu msingi, kama vila unapoishi na unachopenda kufanya.

Kiwango cha A2 – Kutoa taarifa msingi
Unaweza kuzungumzia mada msingi na kusema haja zako - kama vile unapofanya ununuzi.

Kiwango cha B1 – Dhibiti hali za kila siku
Unaposafiri nchini Ujerumani, unaweza kukabiliana kwa urahisi na hali nyingi unazokumbana nazo. Unaweza kuzungumzia hali zako na kutoa maoni yako vyema.

Kiwango cha B2 – Kushawishi
Unaweza kuwasiliana papo kwa papo na kwa ufasaha - hata katika mazungumzo marefu na wasemaji wenyeji. Unaweza kufuatilia maandishi na majadiliano tata na kutoa maoni yako kuhusu mada dhahania.

Kiwango cha C1 – Kuwasiliana kwa uhuru
Huhitaji kutafuta maneno na unaweza kuzungumza Kijerumani kwa vyema na bila tatizo katika hali yoyote. Unaelewa maandishi marefu na yanayotatanisha.

Kiwango cha C2 – Toa maagizo
Unaelewa kila kitu unaochsoma na kusikia na unaweza kuwasiliana papo kwa papo na ufasaha, kutoa taarifa yenye maelezo ya kina.