Mfalme wa Ubeligiji atatua mzozo wa kisiasa katika miliki yake | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mfalme wa Ubeligiji atatua mzozo wa kisiasa katika miliki yake

BRUSSELS:

Mfalme wa Ubeligiji amemteua waziri mkuu wa zamani –Guy VERHOFSTADT aendelee na serikali ya mpito yenye lengo la kuiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.Serikali ya mpito inaapishwa hii leo. Serikali ya muungano wa vyama vitano, inamaliza mvutano wa kisiasa ambao umeendelea kwa mda wa siku 195. Mgogoro huo umezusha tetesi kuwa huenda Ubelgiji ikagawanyika baina ya majimbo yanayozungumza kifaransa na Kiflemish.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com