Mexico City. Rais Bush amaliza ziara yake ya Latin Amerika. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mexico City. Rais Bush amaliza ziara yake ya Latin Amerika.

Rais wa Marekani George W. Bush ameahidi kufanyia mageuzi sera za nchi yake za uhamiaji. Bush amesema hayo mwanzoni mwa mkutano wake na rais wa Mexico, Felipe Calderon, mjini Mexico City.

Suala la uhamiaji linaonekana kuwa suala muhimu la mahusiano kwa Mexico, ambayo ina mamilioni ya raia wake wanaofanyakazi bila kuwa na ruhusa nchini Marekani. Mexico ni kituo cha mwisho katika ziara yake ya siku saba ya mataifa ya Amerika ya kusini. Kumekuwa na maandamano katika kila kituo cha ziara ya rais Bush.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com