1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MEXICO CITY: Rais Bush aendelea na ziara yake ya Amerika Kusini

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJT

Rais George W Bush wa Marekani yumo nchini Mexico katika awamu ya mwisho ya ziara yake ya wiki moja ya Amerika ya Kusini.

Rais Bush anatarajiwa kukutana na rais wa Mexico, Felipe Calderon, kuzungumzia maswala nyeti kama vile uhamiaji, kudhibiti eneo la mpakani na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Maandamano yamekuwa yakifanywa kila mahali rais Bush alipotembelea na rais wa Venezuela Hugo Chavez amemshambulia vikali kiongozi huyo.

Rais Chavez amezuru eneo hilo sambamba na ziara ya rais Bush kuzungumzia dhidi ya kile anachokiita kuingiliwa kwa ufalme wa Marekani.