Mexico City. Mafuriko yaleta maafa makubwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mexico City. Mafuriko yaleta maafa makubwa.

Mamia ya watu wanakimbia eneo la jimbo la kusini mwa Mexico la tabasco baada ya siku kadha za maafa makubwa ya mafuriko na kusababisha kukatika kwa huduma ya maji na umeme. Zaidi ya watu milioni moja wameathirika na mafuriko hayo katika jimbo la Tabasco, ambayo yamesababishwa na kimbunga Noel. Serikali ya Mexico imekiri kuwa kiwango cha maafa haya kimewashangaza na kwa wale ambao bado wamekwama katika maeneo ya vijijini misaada bado haijawafikia.

Wakati operesheni kubwa ya uokozi ikiendelea , kuna hofu kuwa magonjwa yanaweza kusambaa na watabiri wa hali ya hewa wanatabiri kunyeshwa mvua zaidi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com