Messi au Ronaldo? mabishano yasababisha kifo | Michezo | DW | 07.03.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Messi au Ronaldo? mabishano yasababisha kifo

Wengi huwa tunabishana hasa pale vijiweni, ni nani mkali kati ya mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Lakini kuna ukomo wa mabishano hayo

Polisi nchini India imesema mwanamme mmoja ameshtakiwa kwa kumuuwa rafiki yake baada ya kuzuka majibizano makali kuhusu ikiwa Lionel Messi au Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora duniani.

Imesemekana kuwa raia huyo wa Nigeria alimchoma na kipande cha glasi na kumuua Mnigeria mwenzake baada ya marafiki hao wawili kuzozana kuhusu ni nani mkali kati ya Messi na Ronaldo. Kisa hicho kilitokea jana katika kitongoji cha Nallasopara, kaskazini mwa mji wa Mumbai.

Inspekta wa polisi Kiran Kibadi amesema Michael Chukwuma mwenye umri wa miaka 21 anazuiliwa na polisi baada ya kumuuwa Obina Durumchukwu mwenye umri wa miaka 34. Hakuna aliyezungumzia kisa hicho katika ubalozi wa Nigeria mjini New Delhi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com