Messi asaini mkataba mpya na Barcelona | Michezo | DW | 16.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Messi asaini mkataba mpya na Barcelona

Lionel Messi amesaini mkataba mpya uliobora zaidi na klabu ya Barcelona. Mshindi huyo mara nne wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka sasa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mnono zaidi ulimwenguni

Barca haijatoa maelezo zaidi kuhusiana na mkataba huo, ambao unachukua nafasi ya ule wa sasa uliokamilika mwishoni mwishoni mwa Juni 2018, lakini wanatarajiwa kuwa wameiboresha hadhi ya Messi kama mmoja wa wachezaji wanaolipwa kitita kikubw acha pesa katika soka ulimwenguni.

Na hayo yanajiri wakati Barcelona ikiwakaribisha leo Atletico Madrid katika mchuano wa kufa kupona utakaoamua mshindi wa ligi msimu huu.

Atletico sasa watahitaji tu sare watakapokutana na Barca, lakini kama Barca watapata points tatu, basi wataweza kulihifadhi taji lao kwa sababu watakuwa na points 89 kila mmoja, ila tu Barca watatawazwa mabingwa kwa sababu ya rekodi ya kuzilinganisha timu hizo mbili ambayo hutumiwa kuamua mshindi.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman