1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MESEBERG : Wito kuwepo uwazi masoko ya fedha

10 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQz

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa leo wametowa wito wa kuwepo kwa uwazi zaidi katika masoko ya fedha ya kimataifa.

Sarkozy amesema katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Merkel kwenye kasri nje ya Berlin kwamba hawawezi kuruhusu walanguzi wachache kuuangusha mfumo huo mzima wa kimataifa, kukopa katika mazingira yoyote yale wapendayo na kununuwa kwa bei yoyote ile watakayo na bila ya kujuwa nani anayekopesha.

Sarkozy amesema wanapendelea kuwepo kwa uwazi na taratibu kwenye masoko ya fedha na kwa ubepari ambao unawanufaisha wafanyabiashara na sio walanguzi.

Merkel kwa upande wake pia amesema wanahitaji uwazi zaidi kwenye masoko hayo ya fedha.