Merkel ziarani barani Afrika | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.07.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Merkel ziarani barani Afrika

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amewasili Nigeria, kituo cha mwisho cha ziara yake barani Afrika.

default

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel

Leo Merkel, anatazamiwa kukutana na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan. Nigeria iliyo na idadi kubwa kabisa ya watu barani Afrika, ni mzalishaji mkubwa wa nane wa mafuta kote duniani, lakini nchi hiyo ina upungufu mkubwa wa umeme.

Wakati wa ziara hiyo nchini Nigeria, Merkel anatazamiwa kuunga mkono ushirikiano katika sekta ya nishati na malighafi, kama alivyofanya wakati wa ziara yake nchini Angola, kituo cha pili cha ziara yake barani Afrika. Alipokuwa Angola, aliunga mkono kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya Ujerumani na Angola. Alisema kuwa Ujerumani, ingependa kuwekeza katika sekta za miundo mbinu, viwanda na elimu.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und der Praesident der Republik Angola, Jose Eduardo dos Santos (M.), schreiten am Mittwoch (13.07.11) im Praesidentenpalast in Luanda die Militaerischen Ehren ab. Bundeskanzlerin Angela Merkel hat Angola Hilfe bei den Verteidigungsanstrengungen des Landes angeboten. Bei ihrem Besuch in der angolanischen Hauptstadt Luanda sagte Merkel am Mittwoch, denkbar sei beispielsweise Hilfe bei der Ertuechtigung der Marine. (zu dapd-Text) Foto: Clemens Bilan/dapd

Kansela Merkel(kulia) na Rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos

Vile vile Ujerumani ingeweza kushirikiana kutafuta mali ghafi zaidi nchini humo. Merkel alitamka hayo baada ya kukutana na Rais wa Angola José Eduardo dos Santos katika mji mkuu wa Angola, Luanda. Merkel alieanzia ziara yake nchini Kenya, amefuatana na Waziri wa Kilimo, Ilse Aigner na ujumbe wa wafanyabiashara.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com