1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel kuzuru mataifa matatu ya Afrika

Sekione Kitojo
9 Oktoba 2016

Kansela Angela Merkel anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini Mali, Niger na Ethiopia kuanzia Jumapili. Akiwa Mali atatembelea wanajeshi wa Ujerumani wanaotoa mafunzo kwa wenzao wa Mali.

https://p.dw.com/p/2R2v3
Deutschland Tag der Deutschen Industrie 2016 Rede Merkel
Picha: Reuters/F. Bensch

Kansela wa Ujerumani Angela  Merkel ametoa  wito wa kuwa hali bora  zaidi  kwa uwekezaji wa binafsi katika  mataifa  ya  Afrika  ili kuweza  kupambana  na sababu zinazopelekea uhamiaji  wa kiuchumi. Amssema  hayo kabla ya  ziara yake ya  siku  tatu  katika mataifa  ya  Afrika  inayoanza Jumapili(09.10.2016).

Ujerumani  ina  lenga  kurejesha  uhusiano wake  na  bara  la  Afrika baada  ya  mzozo  wa  wakimbizi. Sehemu  ya  mpango  huo  ni kutuma  vikosi  vya  jeshi  la  Ujerumani  kusaidia  kuweka  uthabiti katika  bara  hilo.

Kansela Angela Merkel  ni  kiongozi wa  kwanza  wa  serikali  ya Ujerumani  kwenda  mali. Niger na  Ethiopia  pia  zimo  katika  orodha ya  nchi  atakazofanya  ziara   hiyo  ya  siku  tazu, kuanzia  mwishoni mwa  juma  hili.

Katika hali  ya  kushitua inayotanabahisha  kuhusu  hali  tete  katika eneo  hilo, wanajeshi  22  waliuwawa  na  watu wanaoshukiwa  kuwa wapiganaji  wa  jihadi  nchini  Niger  siku  ya  Alhamis. Shambulio hilo lilifanywa  dhidi  ya  kambi  inayowahifadhi  wakimbizi  wa  mali ambao  wamewakimbia  wanagambo  wa  Kiislamu   nchini  mwao.

Transallmaschine wartet auf dem Flughafen von Bamako auf die Sahara Geiseln, Mali
Wanajeshi wa jeshi la Ujerumani katika uwanja wa ndege wa Mali, BamakoPicha: AP

Wakati  ziara  yake  ikikaribia , kiongozi  huyo  wa  Ujerumani amesisitiza  kwamba  uthabiti  wa  Umoja  wa  Ulaya  unategemea sana  kasi  ya  maendeleo  katika  bara  la  Afrika. Misaada  zaidi  ya maendeleo  inahitajika, sera  mpya  ya  maendeleo  ni  muhumu, uwekezaji  katika  bara  hilo unahitajika  kuongezwa na  msisitizo mkubwa  uwekwe  katika  utawala bora, Merkel  amesema. Alikuwa akitoa  hotuba  katika  chama  cha  wauzaji  wa  jumla  na wasafirishaji  nje  bidhaa  nchini  Ujerumani  mjini  Berlin.

"Kwa ujumla , tunalazimika  kuweka mtazamo  wetu  katika  bara  la Afrika  katika  njia mpya  na  tofauti," kansela  alisema.

Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ujerumani  Frank-Walter Steinmeier  aliitembelea Mali  na  Niger  mwezi  Mei mwaka  huu. Nchi  hizo  zote  mbili  ni sehemu  ya  kituo  cha  kupitia  wakimbizi wengi  kutoka  mataifa  yao  ya  Afrika  magharibi wakitafuta  kufika Ulaya.

Niger  na  Mali zinakabiliwa  na  changamoto  ya  ugaidi  wa kimataifa.

Vikundi  vya  kigaidi , kama al-Qaeda, vinagharamia  shughuli  zao kwa  fedha  kutokana  na  utekaji  nyara  na  biashara  ya  madawa ya  kulevywa  katika  eneo  hilo  la  Sahara.

Baada  ya  mapinduzi  ya  kijeshi  nchini  Mali mwaka  2012, mamia kwa  maelfu  ya  watu  walikimbia  makaazi  yao  kwasababu  ya kutokuwa  na  uthabiti , ukosefu  wa  usalama  na  ukosefu wa  njia sahihi  za  kupata  chakula  na  maji  safi  ya  kunywa. Katika  nchi jirani  ya  Niger , magaidi  wa  kundi  la  Boko  Haram, kundi  la wanamgambo  lililoko  katika  nchi  jirani  ya  Nigeria, limekuwa  na harakati, ambazo  zimesababisha  kuharibika  kwa  usalama  katika nchi  hiyo.

Haja ya  uhamiaji

Denis Tull kutoka  taasisi   ya  Ujerumani  kwa  ajili  ya  masuala  ya kimataifa  na  usalama   iliyoko  mjini  Berlin  ililiambia  shirika  la habari  la  DW  kwamba  wahamiaji  kutoka  Afrika  kupitia  bahari  ya Mediterania ni  suala  la  umihumu  mkubwa  kwa  Ujerumani. "Katika nchi  kama  Mali  ama  Senegal, uhamiaji  ni  jambo  la  kawaida, ni suala  la  utamaduni  wa  jamii, ikiwa  ni sehemu  ya  utambulisho  wa mtu  na  makuzi  yake,"  amesema . Ni  kitu  ambacho  kinaweza  tu kuzuiwa  kwa  taabu  kubwa.  Tofauti  kati  ya  eneo  la  kaskazini mwa  Afrika, Sahel  na  Ulaya  ni  kubwa  mno  kwamba  haja  ya kuhamia  haitapotea. "  aliongeza. Misaada  ya maendeleo haitasababisha  kufutika  kwa  uhamiaji. Njia  bora  inayoweza kufikiwa  inaweza  kuwa  uimarishaji  wa  ushirikiano  wa  hivi  sasa kati ya  mataifa.

Hii  itaonekana  kuwa  kile  Merkel  alichonacho katika  mawazo yake. Anataka  kupanua  miradi  iliyopo  ya  maendeleo, kusaidia juhudi  za  kujenga  miundo  mbinu , kuwapa  mafunzo  na utengenezaji  wa  nafasi  za  ajira, kwa  mujibu  wa  taarifa   kutoka katika  ofisi  ya  kansela.

Rettung von Flüchtlingen im Mittelmeer
Wahamiaji kutoka bara la Afrika wakiokolewa katika bahari ya MediteraniaPicha: DW/K. Zurutuza

Hata  ongozana  na  ujumbe  wa  biashara. "Kwa  kuwa  hatuna maslahi  ya  kiuchumi  na  Mali, tutaangalia  njia  nyingine  ya ushirikiano. Kiwango  cha  biashara  na  Mali  ni  kidogo  mno," Merkel amesema.

Kuhusika  kwa  Ujerumani  kijeshi  kunaweza  kusaidia  kuleta uthabiti  katika  eneo  la  Sahel , Tull alisema. Ujerumani  ina  lenga kujenga  kituo  chake  cha  jeshi  nchini  niger, ambacho  kitatoa msaada  kwa  MINUSMA, ujumbe  wa  Umoja  wa  Mataifa  wa kulinda  amani  nchini  Mali. Vikosi  vya  jeshi  la  Ujerumani  tayari vinashiriki  katika  ujumbe  wa  MINUSMA  pamoja  na  ujumbe  wa kutoa  mafunzo  ya  kijeshi  wa  Umoja  wa  Ulaya  (EUTM). Merkel atafanya  mikutano  na vikosi  vya  Ujerumani  katika  uwanja  wa ndege  wa   Mali , Bamako.

"Upanuzi  wa  shughuli  za  kijeshi  za  Ujerumani  katika  eneo  la Sahel  ni  hatua  moja  mbele kwa  Ujerumani  wakati  ikijaribu kujiweka  katika  nafasi  kwa  njia  mpya  katika  bara  la  Afrika," alisema  Oswald Padonou  kutoka  wakfu  wa  Konrad Adenauer. Yuko  katika  ofisi  ya  kanda  ya  taasisi  hiyo  inayojaribu kukusanya  mawazo  ya  Ujerumani  mjini  Abidjan , Cote d'Ivoire, ambako  anaendelesha  mipango  ya  usalama  na  utawala  bora katika  Afrika  kusini  mwa  jangwa  la  Sahara.  Ujerumani  ilikuwa imejiweka pembezoni  kwa  muda  mrefu.

Lakini  Ujerumani  yenye  uchumi  mkubwa  barani  Ulaya, ikiwa  na nia  ya  kuwa  ujumbe  wa  kudumu  katika  baraza  la  Usalama  la Umoja wa  mataifa,  haiwezi  kuendelea  kuwa  katika  hali  kama hiyo  tena. "Ujerumani  ni  lazima  iwe  na  uwezo  kuweka  msimamo wake  katika  masuala  ya siasa  za  dunia,  hususan  katika  bara  la Afrika, ambako  masuala  ya usalama  ni  muhimu," Padonou amesema.

Kituo  cha  mwisho  katika  ziara  ya  Merkel  ni  Ethiopia. Hii  ni  nchi ambayo  imekosolewa  sana  kwasababu  ya  ukiukaji  wa  haki  za binadamu. Mjini  Addis Ababa , Merkel , atafungua  jengo  jipya  la Umoja  wa  Afrika  lililojengwa  kwa  fedha  kutoka  Ujerumani. Pia anataka  kupata  hisia  ya  hali  ilivyo  katika  nchi  hiyo  binafsi  kwa kuzungumza  na  maafisa  wa  serikali  na  wawakilishi  wa  vyama vya  kijamii.

Äthiopien Anti-Regierungs-Protesten
Waandamanaji wakiandamana kupinga serikali nchini EthiopiaPicha: REUTERS/T. Negeri

Katika  maandamano  ya  Waethiopia  wanaoishi  nchini  Ujerumani katika  mji  mkuu  Berlin, mmoja  wa  washiriki  wa  maandamano hayo  alimtolea  wito  kansela  kuchukua  ujumbe  wake  wa maandamano  na  kuuwakilisha  Ethiopia  na  kuweka  mbinyo  kwa serikali  ya  nchi  hiyo. " Watu wanakufa kila  siku  kule. Lakini wanapambana , kwa  maandamano  na   kuweka  vizuwizi. Siku ambapo  watu  watatauwawa  kwa  kupigwa  risasi  hovyo zimekwisha," alisema. Hii ni  hali  ambayo  Ethiopia  ni  lazima itambue. "Serikali  ya  Ethiopia  haiwezi  kubembelezwa  tena."

Mwandishi : Sekione  Kitojo / zr /DPA

Mhariri: Sudi Mnette